Hawa jamaa wa Chadema wanafundisha watu kuzomea, kunywa viroba, kuandamana na uhuni mwingine mwingi. Wanachosahau ni kwamba hao wanaowafundisha hayo wakitulia wataanza kuyatumia dhidi yao;
Historia inatuonyesha hivyo.
Lakini ninachoshangaa ni kwanini wakikorofishana wao ndani ya Chadema wanasingizia CCM?
Sisi tukikorogana, hatusingizii Chadema. Tabia ya ajabu sana.
Uchakachuaji wa picha walianza nao muda na walianzia na kudarasi picha za mikutano ili ionekane kuwa na watu wengi, hawakujua wanaofanya kuwa wanaendeleza elimu na sasa wameanza kutumika kuwashughulikia wenyewe?
Sababu kubwa ni infighting ndani ya chadema, kundi moja linararua kundi jingine kwa kutumia IT.
Zitto Kabwe ameraruriwa kwa IT, kwanini kundi lake wakae kimya? Wanajibu mapigo, tulieni tu, tutaona mengi, video! nk......
Hii Tabia itakoma tu kwani Wanzania wanazidi kujifunza Upuuzi huu na kugundua Ukweli wa Siasa hizi zisizo wasaidia Wanzania bali kuwapoteza kwa Hali na Mali.
Tizama Mtanzania mwenzangu Nchii hii imekuwa ni nchi ya kila siku kuishi kwa Skendo tena Skendo za Mambo ya Kipuuzi tu, Kila kukicha wanatutengenezea Kisa cha ajabu tu afu Media zinaandika, Watangazaji wanaikomalia kwa kuzungumzia na kuipa Airtime yakutosha wakati hakuna Tunachojifunza wala kutusaidia sisi kama watanzania wa Kawaida, Kuwa makini sana na Siasa Chafu za CDM.
Lakini kuwa makini kwa Kila ukifanyacho Mtanzania mwenzangu kuwa na Choice na Maamuzi ya Maisha yako mwenyewe, Kwani Tizama CDM wanatumia Muda na Nguvu nyingi sana kuhakikisha kuwa wanawashawishi watanzania kwa Uongo, Skendo, Vituko nk..
Lakini Mbaya zaidi wanatumia Kauli chafu, Nguvu kwa Kuumiza , Kuandamana, Kugoma, Kushutumu na kufanya Uongo mwingi ilimradi tu wapate Madaraka kitu ambacho si kizuri kwani Kiongozi waukweli haitaji kumshawishi Mtu..
Mafanikio Makubwa yanayofanywa na Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi wanayaona na yanawaogopesha kwa kuona kusikia na kupata sifa nzuri hata kwa watu wanchi nyingine na ndio sababu inayowafanya wakose hoja za msingi kuzungumza wanabakia kusema uongo kushutumu na kututengenezea Skendo za Ajabu ajabu na kutufanya watanzania tuache kufanya kazi na kujenga Taifa tubakie kununua magazeti ya udaku kama Tanzania Daima ili kusoma uongo uongo wao.
UKWELI ni kwamba, Chadema Nguvu Ya Umma hakina Mashiko, Sera, Hoja, wala Mipango Chanya kwa watanzania ndomana wamekalia Kungoja Tatizo litokee, au waliunde na kulichukua kama Mada na Hoja yakuzungumza kwa Watanzania na kama ni Tatizo kwa Jamii basi inakuwa Gia yakuombea Pesa Ulaya na Pesa Hatujui wakipewa wanatumiaje kwani Tukihoji Tu, Tunapigwa.
#KidumuChamaChaSiasa yaani Chama Cha Mapinduzi
Post a Comment