Home » » Yaliyosemwa na Mwigulu Nchemba na Peter Msingwa Kujibu kuhusu Zitto na CDM

Yaliyosemwa na Mwigulu Nchemba na Peter Msingwa Kujibu kuhusu Zitto na CDM

Written By peterdafi.blogspot.com on Saturday, November 23, 2013 | 1:57 AM


 Peter Msigwa asema ivi
Shame kwa Mwigulu nchemba anatuponda chadema halafu hoja yake yote amejenga kwa kutumia quotation yangu, AKILI NDOGO KUTAWALA AKILI KUBWA,Kama ni mwuungwana na msomi walau angeninukuu, ,Mwigulu utatuelewa tu,
 
Kuvuliwa vyeo kwa Zitto Zuberi Kabwe na Dr Kitila Mkumbo kutakuwa na visingio vingi, ukweli ni kwamba "NDANI YA CHADEMA AKILI NDOGO INATAWALA AKILI KUBWA" It is natural kwamba akili ndogo ikitawala akili kubwa,
1) Yatatumika mabavu na nguvu nyingi kuizuia akili kubwa kupanda juu,
2) Zitatafutwa sababu nyingi na visingizio uchwara kuhalalisha kuizima akili kubwa tofauti na vigezo vya hoja kwakuwa akili ndogo haiwezi kuizidi akili kubwa kwa hoja,
3) Hutumika vitisho vingi kuzuia akili kubwa kuchukua hadhi yake
4) Akili ndogo ni rafiki wa akili ndogo mwenzake, hivyo akili ndogo huzungukwa na akili ndogo kwakuwa ushauri wa akili kubwa akili ndogo hushindwa kutumia ama kushindwa kuonesha umiliki mbele za watu. Kwenye chadema wenye akili wote wako nje ya uzio wa chemichemi ya mawazo. Pale bungeni watu wanaoweza kufundisha na waliokuwa wakifundisha hata unaibu waziri kivuli hawapati kwakuwa wanatumia akili zaidi badala ya nguvu. Lakini walioishia kidato cha kwanza, pili, tatu na zero ndio think tanks na ndio majembe ya chadema kwakuwa wanatumia mabavu na manguvu zaidi kuliko akili sawasawa na matakwa mahitaji ya akili ndogo inayoongoza akili kubwa. Vijana wahitimu wa vyuo wanaopenda siasa waliandikiwa barua kuwazuia kuhutubia mkutano wowote wa hadhara sawasawa na matakwa ya akili ndogo inapotawala akili kubwa. Zito, Kitila, Christowaja, Matiko, Opulukwa, Baregu, Leticia, Selasini, Arfi, Akunay, Naste wengi wao MA holders kwa chadema ni rejects. Ukiwa mwanafamilia au ukoo au kazi au wito maalum wa viongozi ndio utakwepo kwenye list. I know Zitto tangu tukiwa chuoni, he is a brilliant and consistent politician, namjua Dr Kitila tangu chuoni, he is resourceful. Hivi kosa walilofanya ni kubwa kuliko mchango wao waliofanya kwenye kuwajenga watanzania kuwaamini vijana kwenye siasa? Je kosa lao ni kubwa kuliko mchango wao unavyohitajika? Vijana tuko kazini na wakati huohuo tuko mafunzoni. Sio adhabu nzuri ya kuwafukuza ama kuwaondoa kwenye fursa ya kujifunza zaidi. Haya ndio madhara ya AKILI NDOGO KUTAWALA AKILI KUBWA, HOFU NDIO HUTAWALA
Peter Msingwa 
Wanachama na wapenzi wa CHADEMA IRINGA naTanzania kwa ujumla, tumefanya maamzi ya mhimu na yaliyotulazimu kuyafanya kwa faida ya Chama chetu ,na tutaendelea kufanya Kama ni lazima ili kulinda na kukijenga Chama chetu kuelekea uchaguzi mkuu. Niseme tu Chadema iko na itakuwa imara zaidi bila kujali umaarufu wa mtu,tuendele kukijenga na kukiimarisha Chama chetu. CHADEMA NI BORA ZAIDI KULIKO MTU MMOJA MOJA.HATUTARUHUSU MTU AFANYE KAZI YA CCM KWA KUTUMIA JUKWAA LA CHADEMA.
 
Tunawashukuru watanzania kwa kufuatilia kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Nawapa pole wote waliokwazwa na jambo hili, na ninawashukuru wote walionipa pole na kunitia moyo. Ninawashukuru pia walionilaumu na ni vizuri kunyosheana vidole na kuwekana sawa pale ambapo moja wetu anaonekana kukwamisha harakati za mabadiliko.

Haya ni mawimbi katika harakati za mabadiliko na ninaamini yatapita na hayatayumbisha mchakato wa kusimika mfumo wa demokrasia hapa nchini kwetu.

Ninashauri tuwe na subira katika kutoa hitimisho na hukumu katika jambo hili. Mpaka sasa tumekwisha kupata upande mmoja juu ya kilichotokea. Vuteni subira nasi tuseme ndipo mpitishe hukumu. Mungu akijalia tutakuwa na mkutano na waandishi wa habari wakati wowote kabla ya wiki ijayo na tutaeleza upande wetu, na hasa kutoa maoni yetu juu ya kile kilichotamkwa jana kwamba sisi ni wahaini na wahujumu ndani ya chama chetu.

Kwa sasa tambueni tu kuwa mie binafsi bado nipo imara katika kuhakikisha kwamba siwi kikwazo na ninachangia kikamilifu nguvu zangu katika harakati takatifu za mabadiliko hapa nchini.
 
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger