Aliyekuwa mwenyekiti wa chadema mkoa wa Arusha Samson Mwigamba amesema
kuwa mpango unaofuata kwa sasa ni kumuondoa Dr slaa ndani ya chadema.
amesema baada ya zitto kuondolewa ndani ya chama mtu atayefuata katika
kushughulikiwa ni Dr Slaa ambaye kwa sasa amekuwa amekuwa akifanya
shughuli za chama kwa kupelekwa pelekwa bila yeye mwenyewe kujua.
Mwigamba amesema kuwa upo mkakati kabambe unaendeshwa na baadhi ya watu
kwa kushirikiana na watu walio nje ya chama ili kukimaliza chama kabla
ya kufika kwenye uchaguzi mkuu 2015.
Amesema kuwa Mwenyekiti wao Freeman Mbowe ambaye yupo karibu sana na
mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ndio vinara wa mkakati wa
kukiangamiza chama, huku John mnyika na Tundu Lissu wakijiweka mbele
bila kujua hatima yao.
No comments:
Post a Comment