Viunga vya mahakama kuu vimetulia, watu wakiendelea kuwasili tayari kwa usikilizwaji wa pingamizi la Zitto Kabwe kutaka kamati kuu ya chadema isijadili utetezi wake,
Tumejiandaa vema kuwaletea kinachojiri na kuzuia upotoshaji mkubwa uliofanywa jana na kundi la wasaliti hawa wa mageuzi,
NB
Kamati kuu ya chadema inaanza kikao chake kama kawaida hivi punde na Zitto ataanza kutajwa ndani ya vikao hivyo baada ya saa tatu kamili asubuhi hii,
Pipoooooz!!!!!!!
UPDATES
Bado ukumbi wa kusikiliziwa shauri husika haujapangwa, nimeelezwa na mapokezi kuwa hivi punde watapanga na shauri litaanza kusomwa saa tatu,
Makamanda wengi wamashawasili, pikipiki zenye bendera za chadema zimetanda mahakamani,
Hali ya hewa ni nzuri ambapo nyuzi joto linakadiriwa kuwa 26 tu hivyo makamanda waliovalia suti wapo salama kabisa,
Tunaendelea .....
APDATES
Zitto yupo hapa mahakamani tangu saa 12 asubuhi, amejificha kwenye gari aina ya Carina no T564 CAS, anawalinzi wa nne wenye miili dhaifu (fizikali), kwakumuonyesha kuwa nimemuona, nimeenda kuengemea gari hiyo hiyo na huku napost updates,
Naaaam
Tumeruhusiwa kuingia ukumbini na kila mtu ametakiwa kuandika jina lale kwenye kitabu cha wageni wa mahakama,
Haya Zitto nae ameshushwa kwenye gari na wapambe wake wanne, anaingia sasa nae mahakamani,
Jambo lakufurahisha leo nikuwa Zitto amevaa mavazi ya SANDA,
Yaani meupe kama .....!
Wooooooooiiiiii Zitto anazomewaaaaaa CCMmmmmmmmmm, duuuuuh hii hatari ukumbi mzima umelipuka kwakumzomea, alianza kuwambia watu pipoziii, hahaa watu wakamjibu kwa kumzomea sana,
naaam watu wametulia wakimsubili jaji Utamwa aje akate mzizi wa fitina
UPDATES,
Wakili wa Zitto Bwana Msando ameshawasili, hahaa kaja moja kwa moja kunishika mkono, sijasita, nimemsalimia tena kwakicheko huku nikimwambia leo mnapigwa chini rasmi,
Bado mawakili wa Chadema bado hawajafika, tunawasubiri
UPDATES,
Mwanasheria mashuhuri katika ardhi ya Tanzania ndugu Tundu Lissu ndio anawasili, wapi pipooooooz!!!!
Watu wanashangilia hamna mfanoooooooo!
Heheeee kweli nguvu ya umma ni balaaa
UPDATES,
Wakili Kibatala ameingia, watu wanaendelea kushangilia,
Saaa tunamsubiri jaji Utamwa tu
UPDATES
Mawakili wa pande zote waliitwa ndani kwaajili ya kuambiwa kinachoendelea,
Mh Lisu ametoka na kutuambia tutulie kwa sasa Jaji anaandaa, na shauri la msingi litaanza saa nne, vivyo hivyo ametuasa tutulie tusizomee wala kupiga kelele wasije pata nafasi maccm ya kule ffu na kuvuruga utaratibu wetu wakusikiliza shauri hili,
Makene
Mahakama ipo mapumzikoni kumpa nafasi Jaji kuandika mwenendo wa shauri ulivyofikiwa jana na itarejea saa nne na nusu kuendelea na shauri.
Mahakama ipo mapumzikoni kumpa nafasi Jaji kuandika mwenendo wa shauri ulivyofikiwa jana na itarejea saa nne na nusu kuendelea na shauri.
UPDATES
Tayari jaji ameshaingia watu wanaambiwa wasubiri kidogo wataruhusiwa kuingia ndani ya chumba cha kesi,
UPDATES,
Nimepewa taarifa rasmi kutoka kwa Mh Tundu Lisu kuwa kesi ya msingi itasikilizwa saa sita mchana,
Tuweni wavumilivu, matumaini ya ushindi nimakubwa sana,
Watu ni wengi sana, inatia moyo sana!
UPDATES
Tumeingia mahakamani na sasa tunasubiri uamuzi wa Jaji Utamwa
Pipoooooooozi
UPDATES,
Mawakili sasa wanaingia katika chumba cha kesi,
Mh Lisu anatoa kichekesho, baada ya kuingia tu akawauliza makutano, "mbona hamsimami kwa heshima?" watu wote tukasimama akiwemo Zitto, baada ya hapo Lisu akaanza kucheka basi ukumbi mzima ukalipukawa vicheko
kwiii kwii kwii
UPDATES,
Naaaaam
Maaajabu
Karani anashindwa kusoma jalada anazomewa, amejichanganya kusoma akasema ni kesi kati ya Chadema na ccm,
(kimsingi hajajichanganya kwakuwa ndio tafsiri ya kesi hii)
Tunaamriwa tuzime simu, ukibainika kukaidi amri hii ni miezi sita jela,
Jaji ameshaingia, sasa ni utambulisho wa Mawakili,
Kaanza Msando, kwa lugha ya kiingereza,
Lisu katumia lugha ya kiswahili,
Vuteni subira simu chiniiiiii,
UPDATES
Jaji ameanza kusoma uamzi na kuandika,
UPDATES,
Jaji:
-Zitto ameweka pingamizi kufukuzwa uongozi kinyume na katiba.Amemshtaki katibu Mkuu kwa kumtumia barua ya wito kuhudhuria kikao ambacho ni kinyume na katiba kwa kuwa ana rufaa ngazi ya juu
Jaji:
Kibatala alitaka pingamizi litupwe kwa kuwa halina misingi ya kisheria kwa kuwa taratibu zilifuatwa kwa hiyo akataka pingamizi litupwe
Jaji:
Lissu aliwasilisha hoja kuwa matumizi mabaya ya kutumia vifungu vibaya vya sheria vinakiuka katiba ya nchi ibara ya 107(2)
Jaji:
Bw:Msando hakupinga hakupinga hoja ya matumizi ya vifungu visivyo sahihi
Jaji
Jaji anatoa mfano wa kesi ya JUWATA vs Kiwanda cha uchapishaji ya mwaka 1998
Ambayo mahakama iliona tatizo la matumizi mabovu ya vifungu vya sheria kama athari ya maamuzi
Jaji:
Circar Code book page 227 ya Mahakama kuu ya India ,toleo la 11 mwaka 1980 iliamua kuwa pingamizi linapowekwa ni lazima kanuni zinazoongoza taasisi zisomwe pamoja na sheria zake
Ordera 37 inasema mahakama inatoa injuction kwa ajili ya kuzuia mali zisitumike,zisiharibiwe au kupanguliwa
Lissu alijenga hoja kuwa suala hili halihusiani na properties hata kama ni common knowledge ya reference ya circula book
Pia anasema applicant hakuvunjiwa natural justice
Pia mahakama lazima izingatie kuwa taasisi za kidini,kisiasa au mpira haziamuliwi kwenye civil courts
Ametoa mfano wa Aman Vs Lutheran Church ambayo mahakama iliamua
Paragraph 18 inasema kikao cha kamati kuu ni kuwa kitazuia baraza kuu kujadili rufaa yake.Lissu alijibu kuwa baraza kuu huitishwa kwa mujibu wa katiba na na CC ni surbodinate body
Mabishano ya hoja yanaendelea kati yamawakili wa Chadema vs Msando,
Lissu anaomba kwa interest ya public sasa kiswahili kitumike
Msando amepanic sana, Lissu aliomba kiswahili kitumike kwa public interest.Msando alipoulizwa akaanza kuongea.Jaji akamuuliza nimekuruhusu?Watu wakashangilia
Msando kapoteza umakini kutokana na jaji kuamua kutumia kiswahili na yeye kinamsumbua, watu wameshangilia
Msando
Mabishano.Msando anafanya reference ya kesi ya General Tyre VS HSBC bank kuhusu chanzo cha taarifa maana hakuna mumbukumbu
Pia Paragraph 21.Applicant(Zitto) amesema kuwa amenyimwa haki ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa 22 November 2013 mbele ya baraza kuu.Hoja ya Msando aliyotoa
Itetezi wa Msando,
Pia anaomba mahakama iepushe irrepareble injury unaoweza kutokea.Kuwa applicant ni mbunge kwa msingi wa kuwa mwanachama wa chama cha siasa kama katiba ya Tanzania onavyotaka
Na pia ni mwenyekiti wa PAC hivyo anahofia kama kamati kuu itakaa na kutoa uamuzi utakaopelekea kupoteza uanachama wake matokeo ya uamuzi yatamuumiza beyond recovery na pia wananchi waliomchagua itaumiza waliomchagua
Watu wanafyonza na mnong'ono juu
Pia anadai Katiba ya Chadema kanuni ya 6.5.10 inasema"Baada ya kutoa uamuzi kikao husika kinatakiwa kutoa taarifa kwa ngazi ya juu baada ya siku 14'
Kwa hiyo kusema kuwa taarifa hiyo itakamilika baada ya kupitiwa na kikao. cc cha leo inakiuka katiba
Mosando amemaliza kutoa utetezi wake,
Sasa Mh Lisu amesimama na kuanza kuhibu mapigo,
Lissu anasema reference anayofanya ya barua ya kikao cha kamati kuu haikua kwenye record ya documents zikizowasikishwa
Msando anasima na kusema issue ya barua imekuja kwa kuwa counter affidavit imefika saa tano asubuhi.Kwa hiyo ameiondoa sasa amekubali hiyo reference
Msando anaomba mahakama ipokee ombi la mteja wake kwakuwa ni ya msingi,
.......
Lisu:
Lissu sasa. anasema. katiba ya Chadema ibara ya 7:7:14(t) inasema wajumbe wa CC ni pamoja na wakurugenzi wasiokua na kura.Pia Msando ambaye ni diwani wa CHADEMA kata ya mabogini Moshi anatakiwa afahamu Wakili Kibatala ni mkurugenzi wa katiba na sheria ambaye ni mjumbe wa kamati kuu.Kwa hiyo hoja ya kuwa preliminary point of law kuwa hakuwepo kwenye kikao ni suala la ushahidi na tayari mh.Jaji tayari umeamua hapa kabla kuwa ushahidi si hoja za kesi za pingamizi .Kwa hiyo Peter Kibatala kama alikuwepo kama mkurugenzi au la ni suala la ushahidi
Lisu:
Lissu"Mhe.Jaji nakubaliana na kanuni za msingi za utoaji wa zuio kwamba lazima kuwe na primafacie grounds whether the balance of convinience is in favour of reality.Kwamba muombaji anaweza kupata madhara yasiyotibika.Kwa hiyo mere proof of those conditions will not automatically lead to automatically injuction(Amri ya zuio inayoombwa).
Sheria ni lazima ilinde interests of majority against the interest and comfort of an individual for the sake of balance of convinience
Hoja ya apllicant kama ni kuhofia kutotendewa haki angeleta file mahakama kuu ya kuomba baraza kuu liitishwe na si kuzuia kikao cha kamati kuu
UPDATES,
Mh Lisu anaendelea kupangua hoja,
Wakuu simu inakaribia kukata chaji,
UPDATES
Wakuu ngumi zinataka kupigwa kati ya msando na mashabiki wa chadema,
Haahaaa ngoja nikaamue ugomvi kwanza
Naaam mzozo umeisha, msando tumemuomba arudi ndani ya chumba cha mahakama kuepusha shari,
Watu wanauchungu na chadema sijawahi kuona,
Jamaa anaongea mpaka analia, hahaaa
UPDATES
Mahakama imerejea,
Sasa Msando anaomba doc moja wapo ambayo Lisu aliiwasilisha mahakamani kama sehemu ya kielelezo ikataliwe,
Nyaraka hiyo inasema "Ripoti ya Zitto Zuber Kabwe kuhusu kuvuliwa uongozi ndani ya chama changu"
Msando anasema nyaraka hiyo itaharibu mwenendo mzima wa shauri, anasema kwanza haina uhakika kama nyaraka hiyo ni ya Zitto kweli kwakuwa haina saini yake,
Zingatia nyaraka inayotajwa ni ile taarifa ya Zitto aliyoitoa pale Serena Hotel
Lisu
Nyaraka tajwa ni halali na ipo kwenye kiapo tulichokiwakilisha leo asubuhi,
Vilevile wakili msomi Msando anayo mkononi hapo,
Kitendo cha nyaraka hii kukosekana mezani kwako mh jaji hilo haliwezi kuwa nyaraka hii ni batili,
Hata stakabadhi ya malipo ya kiapo hiki hii hapa, "anampa Msando"
Kwahiyo nyaraka hii ni halali, Labda wakili msomi Msando atusaidie ubatili wake uko wapi?
Msando kimyaaaaa! Jaji anamuomba ajibu,
Viambatanisho vilikataliwa na Wakili msando kwa kuwa havijalipiwa na kupewa mhuri halali wa mahakama
Lissu amepinga na kuchukua risiti za vielelezo vya Msando.Akasema hata hizi risiti hazina vielelezo vyenye malipo halali kwa kuwa pia sio bei halali ya rekodi za mahakama.Baada ya hapo Akamrudishia risiti kwa kumrushia kwa dharau
JAJI:
Mahakama inatoa amri ya kumruhusu Mh Tundu Lisu kutumia nyaraka hizi kama sehemu ya rejea za kesi hii, hivyo imetupilia mbali ombi la Wakili msomi Msando.
Lisu anaendelea kuisoma taarifa ya Zitto ya Serena Hotel,
Anasoma tamko la Zitto alilodai kuwa atafuata taratibu za chama.Na pia alitangaza nia ya kukataa rufaa.Kwa hiyo alisema mwenyewe kuwa atafuata taratibu zote za chama na kwa hiyo alitangaza nia ya kukata rufaa.Sasa hizo taratibu za chama zimefikaje mahakamani?
Pia taarifa aliyoomba ya kamati kuu ili akate rufaa inahitaji kuhakikiwa na chombo kile kile cha kamati kuu.Ziwe certified na sio mara ya kwanza kuchelewa kuhakiki taarifa.Kwa hiyo kwa CHADEMA hakuna jambo la ajabu.
Na kama kuna ushahidi kuwa CHADEMA imekataa hapo kuna hoja.Kwa hiyo taarifa inaandaliwa na hakuna haja ya ugomvi(premafacie case)
Msando kimyaaaaa! Jaji anamuomba ajibu,
Viambatanisho vilikataliwa na Wakili msando kwa kuwa havijalipiwa na kupewa mhuri halali wa mahakama
Lissu amepinga na kuchukua risiti za vielelezo vya Msando.Akasema hata hizi risiti hazina vielelezo vyenye malipo halali kwa kuwa pia sio bei halali ya rekodi za mahakama.Baada ya hapo Akamrudishia risiti kwa kumrushia kwa dharau
JAJI:
Mahakama inatoa amri ya kumruhusu Mh Tundu Lisu kutumia nyaraka hizi kama sehemu ya rejea za kesi hii, hivyo imetupilia mbali ombi la Wakili msomi Msando.
Lisu anaendelea kuisoma taarifa ya Zitto ya Serena Hotel,
Anasoma tamko la Zitto alilodai kuwa atafuata taratibu za chama.Na pia alitangaza nia ya kukataa rufaa.Kwa hiyo alisema mwenyewe kuwa atafuata taratibu zote za chama na kwa hiyo alitangaza nia ya kukata rufaa.Sasa hizo taratibu za chama zimefikaje mahakamani?
Pia taarifa aliyoomba ya kamati kuu ili akate rufaa inahitaji kuhakikiwa na chombo kile kile cha kamati kuu.Ziwe certified na sio mara ya kwanza kuchelewa kuhakiki taarifa.Kwa hiyo kwa CHADEMA hakuna jambo la ajabu.
Na kama kuna ushahidi kuwa CHADEMA imekataa hapo kuna hoja.Kwa hiyo taarifa inaandaliwa na hakuna haja ya ugomvi(premafacie case)
Lisu
Lissu:Hoja kuwa kikao cha kamati kuu kinaweza kutoa maamuzi yenye irrepareble injury haina msingi maana ushahidi uko wapi kuwa kamati kuu ikikaa itamfukuza uanachama?
Lisu
Lissu:Maslahi anayoyazungumzia wakili Msando kuwa wapiga kura wa mteja wake watapata madhara,uenyekiti wake wa PAC na ubunge wake hayalingani na athari ya shughuli za chama kikuu cha upinzani na wanachama wake nchi nzima.Equivoically and categorically where is the balance of convinience?
Anaiuliza mahakama je Ikitokea Kamati Kuu ikitoa onyo kwake je kutakua na madhara yasiyotobika?Yaani irreparable injury?
Je,Akifukuzwa uanachama si siku 90 tu uchaguzi utakua umeitishwa na wapiga kura wa Kigoma watakua na mbunge?Irreparable loss iko wapi?Atakachokosa ni maslahi yake binafsi ya posho tu.Kwa hiyo hakuna hoja .Irreparable loss ni kuangalia maslahi ya wengi kuliko posho zake za Ubunge na uenyekiti wa PAC Tu
Anaendelea..
Lissu ametaka mahakama itupilie mbali pingamizi hili halina msingi
Lisu amemaliza sasa ni Msando tena,
Msando,
Hoja ya Chadema iliyosababisha mteja wangu kuja mahakamani ni mbili tu, kwenye barua ya 26/11/2013 inayosema, "kamati kuu imeadhimia kuchukua hatua zaidi kwa kukuvua uanachama au kukufukuza"
Special Thnks kwa Yericko Nyerere JF kwa Up Dates zote toka Mahakama Kuu.
Alichokisema au Kuandika ZITTO KABWE ktk Ukurasa wake wa FACE BOOK Leo mapema sana.
Nimepeleka
shauri langu mahakamani ili chama kifuate katiba cha chama kwa
kusikiliza kwanza rufaa yangu kwenye baraza kuu kuhusu uamuzi wa awali
wa kunivua nafasi za uongozi. Katika maombi yangu hakuna ombi la chama
kuzuiwa kufanya shughuli zake. Nimeomba mahakama kuzuia kamati kuu
kujadili suala langu mpaka hapo rufaa yangu itakaposikilizwa na kikao
kikubwa zaidi cha chama, Baraza Kuu. Mengine ni propaganda na zipuuzwe.
Mahakama ni Chombo cha kutoa haki na ndio kimbilio la kila raia
No comments:
Post a Comment