Home » » Maelezo ya Dk Lwaitama akisimulia mkasa wake na ndege ya PrecisionAir

Maelezo ya Dk Lwaitama akisimulia mkasa wake na ndege ya PrecisionAir

Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, January 28, 2014 | 7:33 AM

Maelezo ya Dk Lwaitama akisimulia mkasa wake na ndege ya PrecisionAir

Akiwaandikia wanachama katika kundi la Wanazuoni, Mwl Lwaitama amesema:-

Ndugu wanazuoni maelezo niliyotoa mtandao wa wanamabadiliko juzi Jumapili haya hapa chini. Kesho Jumatano kwenye The Citizen , kama wataichapisha makala ya column yangu, ninajadili hoja kuu ya kisanga hiki ambayo ni swala la kutumia Kiswahili kutoa maelezo kwa abiria anayekaa karibu na mlango wa dharura. Yule mhudumu alikuwa jeuri na mwenye kutoelewa maana ya kuwa mhudumu wa ndege lakini nadhani hoja kuu ni kwanini wahudumu wanaelekezwa eti lazima kutoa maelezo ya kufungua mlango wa dharura lazima kutolewa kwa Kiingereza wakati maelezo mengine kwa abiria wote ni kwa Kingereza na Kiswahili?

Tena MIMI NIMEWAHI KUTOA USHAURI kama HUU HUU KWA MHUDUMU MWINGINE safari nyingine na yule mhudumu
alinijibu kwa ukarimu kuwa yeye alikuwa anafuata maelekezo tu na mimi nikampa pole yakaisha. Huyu wa juzi alikuwa apendi kupewa maoni na mtu aliyedhani mtu wa hadhi ya chini sana kwake ...maana nilikuwa kama kawaida yangu naonekana kibabu tu kisichozoea mambo ya usafiri wa ndege.

Kama wahudumu wasingekuwa wamefundishwa kikasuku eti lazima kutoa maelekezo ya kufungua mlango wa dharura kwa Kiingereza hakuna tatitizo sakata llote lisingetokea. Pia rubani naye angetumiabusara na kumtuma afisa wa juu ndani ya ndege kuhoji majirani wa nilikokaa angegundua yule mhudumu alikuwa mwongo tu maana hakukuwepo hata majibizano ya kupaza sauti kabisa... mimi nilibaki mdomo wazi aliponiambia yule mhudumu wa kwanza ninaweza kusimamisha ndege ukatolewa nje kama tishio na mimi nikamjibu kwa upole ya nini yote hayo ndugu yangu maana mimi najua Kiingereza na wewe endelea na maelezo yako kwa Kiingereza... lakini nadhani siku hiyo labda aliamuka vibaya ...Bado sijaamini angeweza kutunga uongo wa eti kuna mtu anafanya fujo vile tu nilitoa maoni yangu tu tena kwa tabasamu langu la kwaida ninapokuwa na huzuni juu ya mambo yasiyo na mantiki yanayotendeka duniani. MAELEZO YANGU YA JUMAPILI HAYA HAPA CHINI.

"Yaliyonikuta Mwanza

Nawashukuru wote kwa kunipa pole. Wanasheria wa rafiki yangu binafsi Dr Antony Diallo, mmiliki wa Star Tv na Radio Free Africa, na wanasheria waliotumwa na Nd. Sungusia wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ( Legal and Human Rights Centre, LHRC) chenye makao makuu Dar es Salaam walifika kituo cha polisi cha kiwanja cha ndege Mwanza na wakafanikiwa kuniwekea dhamana na hivyo niko nje kwa dhamana vinginevyo ningelala selo ndugu zangu _Kesho nitaripoti polisi kufuatilia juu ya kesi iliyofunguliwa dhidi yangu na Precision kama itaenda mahakamani au vipi.

Kilichotokea kifupi ni hivi. Nilipanda ndege Flight PW 0492 iliyotarajiwa kuondoka Mwanza saa 3 dakika 50 asubuhi kuelekea Bukoba. Nilikuwa nimekaa kiti namba 2B na mtafiti mmoja anayefanya kazi Maruku Tea Estate huko Bukoba alikaa kiti na. 2A kwenye dirisha kushoto kwangu. Wakati ndege inaanza kukuelekea inakoruka alikuja mhudumu wa kike akatuuliza na yule mwenzangu kama tunajua Kiingereza na mimi nikasema kwa utani huku nikicheka kuwa tunajua kidogo. Yule muhudumu gafla akatahamaki akasema kama sijui kiingereza aniamishe kiti.

Mimi nikamjibu kuwa hakukuwa na haja maana mimi najua kiingereza maana ni mwalimu wa siku nyingi wa Kiingereza lakini nilichokuwa nashangaa ni kwa nini nyie wahudumu mnapenda kutoa maelezo kwa Kiingereza wakati mgeyatoa maelezo hayahayo kwa Kiswahili mara baada ya kujua kuwa sisi ni Watanzania na tunajua Kiswahili vizuri zaidi kuliko Kiingereza. Binti huyo nikaona ametaamaki na kuanza kusema lazima niteremshwe.

Mimi nilidhani masihala maana niliwahi kutoa ushauri huu hapo nyuma kwa mhudumu mwingine wa Precision Air na yeye alinijibu kwa heshima kabisa kuwa wao maelezo wameambaiwa lazima wayatoe kwa Kiingereza. Mara yule mhudumu wa kwanza akaondoka akaja mhudumu mwingine wa kike akasema kama sijui Kiingereza niamishwe nikamjibu wa taratibu na tabasamu langu la kawaida ninalolitoa katika mazingira kama haya ya dalili za kukosekana busara na mtoa huduma kukimbilia kwenye mambo ya kugombana bila sababu kuwa hakukuwa na tatizo jamani kwani Kiingereza nakijua na nilichokuwa nimempa mwenzake ni ushauri tu.

Yeye wala hata hakuzungumza na mimi tena aliondoka ndipo nikasikia rubani akitangaza eti kuna tatizo la kiusalama na ndege itachelewa kuruka ili litatuliwe. Mara polisi wane hivi na muhudumu wa Precision wa kiume mmoja wakaingia ndani ya ndege na kusimama mbele yangu nilipokuwa nimekaa na kufunga mkanda. Mhudumu akaniambia inabidi au nikuamishwe kiti au ni ushushwe. Wakati huo huo wale polisi wakang'angania eti lazima nishuke. Nikauliza nitii amri ya nanai sasa? Polisi mmoja aliyeonekana kama mwenye kuwaongoza wale polisi wenziwe akainama akanifungua mkanda wa kwenye ndge akaninyanyua mkuku mkuku na kunitoa nje ya ndege.Hata begi zangu mbili za mkononi ilibidi niombe nikiwa chini nipewe.

Abiria waliokuwa karibi na nilipokuwa walishangaa na kusema kwani amefanya nini huyu baba . Lakini waliokuwa nyumba mabali hawakujua kilichotokea zaidi ya manaeno waliokuwa wamelishwa na rubani na wlae wahudu kuwa kuna baba kule mbele amnaleta fujo inabidi ateremshwe. Nikapelekwa kituo cha polisi hapo uwajani huku nikisikia wakinongonezana kuwa lazima kuniweka selo (lockup ).

Nikafanikiwa kumpigia Dr Antony Dialo simu akazungumza nao wale askari na wakaanza kuchukua maelezo yangu nikiwa nimeketi ofisini kwao kwenye kochi walau badala ya kuwekwa lockup... Baadaye nilipigia Ndugu Sungusia wa LHRC na Dr Antony Diallo wote wakanitumia wanasheria walionisaidia kuandika na kutia saini maelezo yangu. Wale wanasheria wakaniombea dhamana nikapata nikaruhusiwa kutoka pale kituoni lakini nikaamriwa kuripoti kituoni pale asubuhi kesho Jumatatu kwa maelekezo zaidi.

Wakati huo ndege ile ya Precision iliondoka ikaenda Bukoba na ikarudi tena baadaye kutoka Bukoba na ndipo nikamuona yule muhudumu wa kike wa pili eti ndiye anatoa maelezo juu ya eti mimi kufanya fujo. Yule muhudumu aliyewadanganya wenzake wote pamoja na rubani kuwa eti mimi nimefanya fujo wala hakutoka nje ya ndege iliporudi kutoka Bukoba kutoa maelezo.

Katika sakata lote ili yule abiria aliyeketi kushoto kwangu siti namba 2A wala hakuhojiwa na rubani wa ndege ile kujiahakikishia kama madai ya eti mimi kufanya fujo yalikuwa ya kweli na wala hata polisi waliotekereza maelekezo ya rubani yakuniondoa ndani ya ndege mkuku mkuku hawakujiangaisha kuuliza yule abiria jirani yangu aliye kuwa siti 2A kama ni kweli mimi nilifanya fujo yoyote au nilitoa maoni tu juu ya matumizi ya Kiswahili katika kutoa maelezo ya juu ya kipi cha kufanywa wakati wa dharura.

Hadi sasa bado sijaelewa kisa kilichomfanya yule mhudumu atahamaki na kunibambikizia tuhuma ya kufanya fujo yarabi... maana hakukuwepo hata na kubadirishana maneno kwa ukali kwa upande wake au wangu. Nimebaki nimeduwaha hadi sasa kuwa hivi ni kweli miaka zaidi ya 50 baada ya uhuru nimekatishiwa safari yangu kwa kutoa maoni tu ambayo mhudumu yule wa shirika la ndege binafsi angeweza kupuuza. Bado sipati maelezo kwa nini haya yalinitokea zaidi ya kuhisi kuwa haya ni matokeo ya mfumo wa kuandaa wahudumu wa ndege wa Precision unaowavimbisha kichwa kuwa kwa kutamka kwa rubani kuwa kuna abiria anafanya fujo hiyo inatosha abiria yule kunyanyaswa kama nilivyonyanyaswa na kudhalilishwa kwa kutuhumiwa kufanya fujo ndani ya ndege. Lazima nikiri hata hivyo kuwa maafisa Kadhaa wa kituo cha polisi cha uwanja wa ndege pale Mwanza walinionesha uungwana sana na walikuwa wakarimu kwangu kuliko hata wahudumu wale wawili wa Precsion Air.
Mwl. Lwaitama"

JANA POLISI Mwanza WALIKUWA WAKARIMU MARADUFU NA WAMENIPA SIKU KADHHA ZA ZIADA ZA DHAMANA WAKATI WAKIENDELEA NA UPELEZI WA KAMA TUHUMA ZILIZOELEKEZWA KWANGU ZILIKUWA ZA KWELI. WATAWAHOJI WALIOKAA KARIBU NA MIMI NA SIMU ZAO WAMEPATA na sina shaka ukweli ukijulikana labda hata Precision watataka kuniomba radhi maana mimi ni mteja wao mkuu.
Mwl. Lwaitama
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger