Home »
siasa
» Mh, JOHN SAMWELI MALECELA ATOA TAMKO KUHUSU TAMKO LA PAUL MAKONDA.
Mh, JOHN SAMWELI MALECELA ATOA TAMKO KUHUSU TAMKO LA PAUL MAKONDA.
TARIFA KWA VYOMBO VY A HABARI JANA 30/01/2014
Ndugu zangu waandishi wa habari, awali ya yote naomba niwasalimie na
niwapongeze kwa kufika mwaka mpya 2014,pia naomba niwapongeze kwa kazi
kubwa ambayo mmekuwa mkiifanya hasa kuhakikisha watanzania wanapata
habari kwa kila jambo linaloendelea kila kona ya taifa letu la Tanzania
Ndugu waandishi wa habari nimewaita hapa ili kuzungumza nanyi na
mnisaidie kufikisha ujumbe kwa watanzania hasa kuhusu jambo hili ambalo
limekuwa gumzo kwa watanzania wengi la mbio za urais 2015 kwa baadhi ya
watu ndani ya chama changu cha mapinduzi (CCM),kilichonisukuma zaidi na
kupata hamu ya kuongea nanyi ni baada ya kumsikia na kumuona kijana
wetu ndani ya chama cha mapinduzi bwana paul makonda akiwa na ujasiri wa
kukemea vitendo mambo haya yanayofanywa na baadhio ya viongozi bila
uwoga wowote naomba tuchukue fursa hii kumpongeza sana kijana huyu.
Nadiriki kusema nampongeza kijana huyu hasa kwa kauli zake nzito na za
kijasiri kwa maslahi ya chama changu cha CCM ili chama kiendelee
kupendwa na kuchaguliwa na watanzania.
Pia itakuwa
si busara kama sitawapongeza vijana wangu katibu mkuu wa chama ndugu
ABDULRAHMAN KINANA na NAPE NNAUYE kwa juhudi zao za dhati za kujenga
chama na kuendelea kuwaeleza wananchi juu ya misingi bora ya chama cha
mapinduzi (CCM)kwa kuwakemea viongozi wasiofaa bila kujali cheo na
umaarufu wao ndani ya chama na serikali,nawaomba waendelee na juhudi
zao hizo nami naziunga mkono juhudi zao na kama kuna watru wanaowabeza
naomba wasijali kwani kukemea viongozi wasiofaa ndani ya chama na
serikali ni msingi wa chama chochote kilichounda serikali.
Aidha nawaomba watanzania wenzangu wazalendo wasikubali kukatishwa tama
na kikundi cha watu wachache wasio na mapenzi mema na taifa letu ambalo
limekuwa mfano wa kuigwa kwa amani,upendo,utulivu na mshikamano urithi
tulioachiwa na baba yetu wa taifa mwalimu julias kambarage nyerere ndani
na nje ya mipaka ya bara letu la afrika.
Ndugu
zangu waandishi wa habari naomba niwaambie kuwa msemaji wa UVCCM kijana
wetu paul makonda namuunga mkono kwa kitendo chake cha ujasiri cha
kumkemea ndugu EDWARD NGOYAI LOWASA bila uwoga kwa jinsi anavyokivuruga
chama chetu kwa lengo la kutaka urais 2015 huku secretariet ya chama
ikiwa imekaa kimya wakati inajua kuwa muda wa kuanza mbio hizi bado na
kufanya hivi kwa sasa ni kukiuka misingi na katiba ya chama.hapa
najiuliza kuwa ile misingi imara ya uongozi ndani ya chama chetu cha
mapinduzi iko wapi?mpaka tumuachie mototo ndio akemee haya?je!hapa chama
kiko wapi?
Ukweli ni kwamba wanachama wetu na
vijana wamekuwa njia panda huku wakitamani kusikia tamko au karipio la
chama juu ya suala hili la harakati za urais 2015 bila mafanikio.
Naomba niseme kuwa bila kuwa na karipio au tamko la chama, hawa
wanaotumia pesa zao hadharani kwa lengo la kutafuta umaarufu na
ushawishi kwa vijana ili kupata madaraka wanaharibu misingi yetu bora ya
uongozi iliyowekwa na waasisi wetu ndani ya chama.
Kinachonisikitisha zaidi ni kuona juhudu za uongozi wa sasa wa chama
ngazi ya juu ikiwa ni pamoja na sekretarieti inayoongozwa na katibu mkuu
ABDULRAHMANI KINANA na katibu mwenezi NAPE NNAUYE za kutetea chama hiki
zinatiwa mchanga.
Ninaomba juhudi hizi zisibezwe na
watu wenye nia njema na chama.,ukweli ni kwamba vijana hawa wamekuwa na
juhudi kubwa sana ya kujenga na kuimarisha chama chetu kwa wananchi
kila pembe ya taifa letu kwa kukemea na kueleza misingi ya uongozi bora.
swali:je! Chama hakioni haya mpaka vijana ndio waone?
Kwa hili ni lazima tubadilike ili kujenga chama chetu na naishauri
secretariet ya chama lazima ichukue hatua mara moja,kijana huyu paul
makonda asingesema haya yote kama hana uhakika wa ushahidi wa wa haya
aliyoyasema na nampongeza sana.
Vijana na wanachama
wengi wa CCM wamekuwa na hamu kwa muda mrefu ya kutaka kujua msimamo wa
chama chao bila mafanikio na ndio sababu ya baadhi ya
wengine kupoteza mwelekeo.
Sisi tulikijenga chama hiki kwa taabu sana hapakuwa hata mtu mmoja
aliyediriki kutumia fedha zake kutaka madaraka.nidhamu,busara na uchungu
wa rasilimali za taifa hili kwa maslahi ya wananchi ndio vilituongoza
kufuata misingi na maadili ya uongozi ndani ya chama na serikali,ndio
maana tunaumia sana kuona chama sasa kinataka kutekwa na wenye fedha kwa
uchu wa madaraka,mpaka tunashangaa na kujiuliza hizi pesa wanatoa
wapi?na haya madaraka wanayotaka kwa kununua ni kwa maslahi ya nani?huku
watanzania wakiendelea kuwa maskini.
Mfano hivi
karibuni baadhi ya viongozi wa chama ngazi ya juu wamejibishana kwenye
vyombo vya habari,vitendo hivi havina tija kwa chama na wala havileti
umoja na mshikamano ambao umedumu ndani chama kwa muda mrefu.
Mwisho Ninaomba sekretarieti ichukue hatua haraka kama alivyoomba
kijana wetu makonda na kweli kuchelewa kuchukua hatua jambo hili
kumejionyesha wazi kwamba utaleta kutokuelewana ndani ya chama kusiko
kuwa na lazima.
MWISHO
JOHN SAMWELI MALECELA
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Post a Comment