Mambo 5 yanayoweza ku Dhuru Ubongo wako.

Kukosa Kifungua Kinywa asubuhi





Watu wanaokosa kifungua kinywa asubuhi wanapata upungufu wa kiwango cha sukari kwenye damu. Hii husababisha upungufu wa madini (nutrients) kwenye ubongo na hatimaye ubongo hudhoofika.

Kula kupita kiasi:
Inasababisha kukaza kwa misuli au mishipa ya Ubongo na hatimaye hupelekea kudhoofika kwa mfumo wa

fahamu.

Kuvuta Sigara:

Kwenye sigara kuna kitu kinaitwa Nikotini ambayo ndani yake kuna chembechembe ambazo zina sababisha makunyanzi kwenye ubongo na kisha kudhoofu.

Kutumia Sukari nyingi:

Matumizi ya sukari nyingi husababisha matatizo katika mfumo wa unyonyaji wa Protini na Madini joto mwilini na kusababisha ugonjwa wa Utapiamlo ambao pia huingilia mfumo wa fahamu

Kuvuta Hewa chafu:

Ubongo ndio mtumiaji mkubwa wa Oxijeni tunayo ivuta. Unapovuta hewa chafu unapunguza mgawo wa Oxijeni kwenye Ubongo na hatimaye kupunguza ufanisi wake