Polisi wakipambana na vijana waliokutwa eneo la msikiti wa Musa.
Vijana wakiwa tayari kupambana na polisi.
VURUGU wakati wa msako wa polisi katika msikiti wa Musa mtaa wa
Majengo, Mombasa nchini Kenya umesababisha vifo vya watu watatu akiwepo
polisi wakati wengine wengi wakijeruhiwa. Vurugu hizo zilitokea kuanzia
juzi Jumapili baada ya polisi kuvamia msikiti huo uliodaiwa kuhubiri
itikadi kali za kiislamu. Katika msako huo vijana zaidi ya 100
wamekamatwa na jana walifikishwa mahakamani kujibu makosa ya kujihusisha
na vitendo cha kigaidi.
(PICHA NA MDAU WA GPL, MOMBASA)
CHANZO:- GPL
No comments:
Post a Comment