Mjumbe
wa Baraza Kuu la Taifa la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
(UVCCM) kutoka Mkoa wa Tanga Ndugu Husna Mbwambo Sekiboko amefunga tawi la
Chadema katika Kijiji Cha Lukozi na kupandisha Bendera ya Chama Cha Mapinduzi
kutangaza Ufalme mpya wa Chama hicho cha siasa.
Tukio
hilo limetokea jana tarehe 6th March 2014 katika kijiji cha Lukozi,
wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga, ambapo sambamba na kuasisi tawi hilo la Chama
Cha Mapinduzi pia kiongozi huyo wa UVCCM ameingiza wanachama wapya 206 ambapo
wengi wao walikuwa ni wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Mjumbe
huyo wa Baraza Kuu la Taifa la UVCCM, alifungua mashina sita yakiwemo ya
Manyara, bodaboda, n.k pia alifanya vikao vinne vya ndani ambapo alizungumza na
wanaCCM juu ya hali ya Uimara wa Chama na kuhoji kasi ya utekelezaji wa Ilani
ya Chama Cha Mapinduzi katika Kijiji hicho ndani ya Wilaya ya Lushoto pamoja na
kufanya mkutano wa hadhara ambao ulihudhuriwa na wananchi wengi wa Lukozi.
Pamoja
na vikao hivyo lakini pia Husna alitembelea vikundi vya ujasiriamali vya akinamama pamoja na kambi ya JUDO ya Vijana
wilayani Lushoto na kujadili nao Changamoto wanazokutana nao na kushirikiana
nao kuzipatia ufumbuzi.
Husna
anafanya ziara za kawaida katika Mkoa mzima wa Tanga katika kuhamasisha Vijana
kujiunga na Chama Cha Mapinduzi pamoja na Jumuiya ya Umoja wa Vijana.
Post a Comment