RASLIMALI, MADARAKA, MIPAKA DHULUMA NA
UTAWALA BORA
Naomba
nichukue fursa hii adhimu ili kuweza kuandika japo kwa ufupi mambo mengi
yanayotokea katika nchi hii, hasa katika ukiukaji wa haki za binadamu ama kwa
sababu ya upofu na umbumbumbu wa sheria wa baadhi ya watawala wetu, Rushwa
miongoni mwa watawala, uzembe wa viongozi na watawala wetu, chuki na visasi
miongoni mwa watawala na masuala mengine kama haya. Nipate kuweka bayana ya
baadhi ya mambo yaliyofichika hasa katika maeneo muhimu yenye neema kwa taifa
ambako, raslimali za taifa zimekuwa zikiondolewa mikononi mwa wanaNchi na
kuwekwa mikononi mwa madhulumati wachache.
Ardhi
ni ralimali muhimu kwa ustawi wa taifa. Ardhi yenye rutuba ni bora kwa shughuli
za kilimo, ardhi yenye madini ni maeneo muhimu ya uwekezaji, na ardhi iliyoko
katika miji, manispaa na majiji ni kwa ajili ya ukuaji na uendelezaji makazi na
miji husika. Miongoni mwa kero kubwa zinazolikera taifa hili na hasa
linalowakera raia wazalendo wa taifa hili Tanzania ni matumizi ya ardhi
yasiyozingatia ustawi wa Mtanzania ambaye ni maskini na badala yake kuzingatia
kuwagawia ardhi yote wawekezaji. Uwekezaji umekuwa ndio mgongo na mbeleko
kubebea wizi, unyang'anyi, rushwa, ufisadi, dhuluma, mauaji ya raia wasiokuwa
na hatia. Mauaji mengi yamekuwa yakitekelezwa ama moja kwa moja, ama kwa jinsi
ambavyo, "wawekezaji" hawawezi kudhibitiwa ili kuzuia sumu kutoka
katika viwanda vyao yasiingie katika mifumo ya maisha ya watanzania.
Tumeshuhudia tafiti mbalimbali zikitangaza kuwa dhana ya uwepo ama wa sumu ama
uhatarishaji wa maisha ya wananchi kutokana na mabaki ya uchafu wa viwanda si
hatari kwa maisha ya wananchi. Tumeyashuhudia haya katika migodi ya madini hasa
dhahabu huko Geita, Kahama, Bulyanhulu, Buzwagi na katika viwanda mbalimbali
huko Dar es Salaam na miji mingine kuliko na viwanda.
Waswahili
tuna Msemo "Kila Mjenga Nchi ni
Mwananchi na Kila Mbomoa Nchi ni Mwananchi". Maana halisi ya usemi huu
ni kuwa, wananchi ndio kila kitu kwa ama ustawi ama ufu wa taifa lolote lile
duniani na kwamba nguvu ya wananchi kwa wingi au uchache wao ni muhimu katika
kusimamia raslimali zilizopo jinsi zinavyotumika, sababu ya kutumika na
mipangilio ya uendelevu wake.
Nimeshika
kalamu kuandika makala haya kwa sababu kuu moja, kuhoji uhalali wa jeshi la
polisi nchini kupiga, kufunga na kutesa raia na viongozi wao kwa kisingizio cha
uvunjifu wa amani huku wao ndio wanavunja hiyo amani kwa sababu zinazoweza
kuelezeka kiurahisi zaidi ukiziita rushwa. Mahali pengi Tanzania tumeshuhudia
viongozi wa watu (Wabunge) walio katika mstari wa mbele kutetea haki za raia
waliowachagua wakiteswa, kuwekwa kwenye rumande za polisi, kufunguliwa mashtaka
na mbaya zaidi hata kudhalilishwa utu wao. Haya yanatokea sana hasa pale
kunapokuwa hakuna maelewano kati ya wawekezaji na viongozi wa wananchi.
Leo
Tanzania tupo katika kipindi muhimu sana cha ustawi wa taifa letu. Ni kipindi
ambacho ama tutaamua mustakabali chanya wa taifa letu, ama ufu wa taifa letu.
Tupo katika mchakato wa kutengeneza katiba mpya, katiba ambayo itakidhi mahitaji
ya Tanzania kwa sasa. katiba ambayo itatambua raslimali za taifa na kuainisha
kwa uwazi bila kificho kwamba raslimali zitatumika kwa ajilia ya manufaa na
maendeleo ya Tanzania na Watanzania. Katika mambo tunayotakiwa kuyaweka sawa ni
umiliki, umilikishaji na umilikishwaji wa ardhi yenye madini kwa wananchi (hasa
wachimbaji wadogo) na uzuiaji ardhi hii kuchukuliwa na serikali kwa namna
ambayo italeta manung'uniko na hata kufikia hatua ya kuhatarisha amani ya nchi.
Kutafsiri ardhi iliyopo kwa matumizi ya wakulima na matumizi ya wafanyakazi na
kutambua maeneo mahsusi kwa kazi hizi. Mauaji tuliyokwisha kushuhudia, ambayo
yametokana na mapigano ya wakulima na wafugaji, yalitokana sana na sababu ya
kutotambua maeneo muhimu wa ajili ya shughuli za wakulima na wafugaji.
Tanzania
ya sasa tunashuhudia nguvu kubwa wanayotumia polisi wetu katika matumizi ya
silaha dhidi ya raia wao eti kwa kigezo kuwa raia wamewazidi nguvu. Matumizi ya
mabomu ya machozi, risasi za moto na aina ya vifaa vinavyotumika kudhibiti wananchi
wasio na chupa za maji tu ni kubwa kuashiria weledi katika jeshi la polisi
haupo tena ama kama upo basi kwa "Maelekezo
maalum" unatumika isivyopaswa. Haya yametokea sehemu mbalimbali mfano
huko Iringa, Mbeya, Mwanza, Mtwara na hivi juzi huko Nzega Tabora ambako Mbunge
wajimbo hilo Mh. Hamisi Kigwangala (HK) alitupwa rumande wakati akiwa kwenye
utekelezaji wa majukumu yake ya kawaida.
Katika
tukio la Nzega, kuna mambo yaliyojitokeza ambayo hayaelezeki ama maana yake
kabisa ama taathira na mwelekeo wa maana yake. Mbunge alitoa taarifa kupitia
mtandao wa jamii "facebook" kuwa....... amenusurika kuuawa....... na
kwamba yule aliyetaka kutekeleza hayo mauaji ndiyo aliyemwambia ...... lakini
kilichomponya HK ni, shabaha ndogo ya Mlenga shabaha (huyo) polisi ambapo
risasi iliyomkosa Kigwangala ilimpata raia (kijana) katika paji la uso.
Mheshimiwa Mbunge aliandika "Nimenusurika
kuuawa muda mfupi, askari kwenye gari ananiambia, bahati yako nilikulenga
kichwa....." Sasa hii aliwataarifu nyie Ndugu zangu lakini mimi nilikuwepo Nae eneo la tukio hii ni hatari sana Jamani.
Mkuu wa Wilaya
hakuwepo wilayani na kwamba hata alipotafutwa alijibu
"Nipo nje ya wilaya
na OCD hajanipa taarifa yoyote nasubiri nipewe taarifa".
Hapa ndipo penye
tatizo,
1.
Je OCD kumkamata Mbunge alitekeleza
agizo la nani, ama katika kutimiza wajibu wake alishauriana na na nani;
2.
Mbunge alikuwa katika utekelezaji wa
shughuli mbalimbali zinazohusu majukumu yake ya kibunge jimboni kwake. Na
kwamba jambo alilokuwa anashughulikia ni mgogoro wa uchimbaji madini uliopo
katika wilaya ya Nzega, je Mkuu wa Wilaya hakuwa na taarifa na hilo hadi
aliposikia Mbunge amekamatwa?
3.
Kinga ya Mbunge inaishia wapi hasa
anapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yake?
4. Kwanini umkamate Mbunge kwa Kumdhalilisha kama vile na tena bila kuwasiliana na katibu au Mwenyekiti wa Bunge?
5. Lakini pia kwanini umkamate na Mwandishi wa Habari kwa kuwepo tu eneo la tukio?
6. Kwanini baadhi ya waandishi walifukuzwa kutishiwa na kusukumwa pia kutusiwa na askari?
7. Kwanini Askari,,,! Askari anamtukana Mbunge kwa matusi makubwa makubwa na kumsukumizia Lumande, kwa jeuli ipi hasa?
8. Je..!! Ni sawa na usemi usemao mti wenye matunda ndo hupigwa mawe! HK amefanya mengi jimboni tena yale ya misimamo na kusaidia wanyonge hii manake Mkoa na Wilaya ya Nzega Viongizi wao Baadhi si waadilifu na wanakiuka Taratibu za Ufanyaji kazi wa Umma?
Nimeamua
kuweka mfano wa tukio la Tabora kama rejea angalau kwa ufupi maana mimi ni
mhanga wa tukio nzima na nililiona lilivyotokea mwanzo hadi mwisho. Taaluma
yangu ya uandishi wa habari ilinipeleka katika mikutano ya mheshimiwa Mbunge,
lakini pia kwa kuwa mimi ni mkazi wa Nzega, nililazimika kwenda katika mikutano
hii. Kwa nafasi yangu ya uandishi mimi ni mwandishi na mmiliki wa blogspot
inayoitwa peterdafi.blogspot.com. na uvccmtz.blogspot.com. Lakini
pia Baada ya Mheshimiwa Mbunge kukamatwa, ilinilazimu kulifuatilia hilo tukio
kwa ukaribu hivyo nililazimika kwenda hadi kituo kikuu cha Polisi Nzega.
Nilipofika tu, nikakamatwa na kuwekwa chini ya Ulinzi eti nilionekana na Mbunge
wakati wa Mikutano. Maelezo kwamba mimi ni mwandishi wa habari hayakusaidia
bali walidai kitambulisho wakati hata aliyekwa ananidai kitambulisho
hakunionyesha kitambulisho. Ushahidi wa kutaka kuifungua blogspot yangu ili
waithibitishe walikataa, hapo nikajua lengo lilikuwa kuniweka ndani.
Nilitoka na Mh. Kigwangalla
Dodoma siku ya jumamosi 22/03/2014 saa 14:45 PM tukajaza mafuta Gari yake na
safari ilianza saa 15:15 PM, Kuelekea Nzega kupitia Igunga ambako Mama yake Dk,
Hamisi Kigwangalla alikuwa amelazwa kwa Kupasuliwa KIDOLE TUMBO, Mama aliugua
Gafla na kulazwa Hospitali ya Igunga, Ikiwa Mwanae alikuwa Nje ya Nchi kwa
Shuguli zake, alikatisha ziara na kurudi Tanzania kwa Kero za WanaNzega
kufukuzwa katika Mashimo yao ya kuchimbia dhahabu. Basi tulifika Hospitali ya
Wilaya Igunga Saa Mbili za Usiku na Kumuona Mama kalazwa akiwa anaendelea Vyema
tu na Matibabu, tulimjulia hali na kisha, Tuliondoka na Kufika Nzega usiku wa
saa 22:30 kisha nikachukua Chumba katika Hotel Moja na kwenda kupata Chakula
Grand Villa hapo, nilimnukuu jamaa mmoja aliekuwa akizungumza habari za
Kuvuruga Mkutano wa Kigwangalla wa Kesho yake Nzega ndogo na kisha uko
Mwanshina Hapo HK alikuwa Nyumbani kwake nimemuacha na nilikuwa na Dereva wake
ambae alisikia habari za kuharibu kikao cha kesho yake nilimjuza HK yote hayo
na Kisha kunukuu kuwa Jamaa alikua akiongea habari za kuvuruga mkutano na kisha
alipokea Simu ya Bashe na kuzungumza nae kifichoni. Kesho yake tulienda Nzega
ndogo tukafanya mkutano wananchi wakatoa malalamiko ya kunyanyaswa kwao na
viongozi, Hapo nilishuhudia Hisia za zawatanzania wakilia kwa kunyanyaswa na
kupokonywa mali zao, inauma sana kuona Mtu mzima akilia kwa uchungu, Mbunge
aliomba askali tuongozane naokuelekea Sehemu Migodi ilipofukiwa kwa ajili ya
kumalizia Mkutano wake wa Pili hapo, Askali walitangulia na kwenda nao wakiwa
wanatulinda kwani watu walikuwa wakitembea kwa makundi makundi tu na kubadilishana
mawazo hapo Mbunge nae alisema "ntatembea
na wananchi wangu kwani wao wanatembea na mimi ntatembea pia" Tulienda na kukalibia sehemu ya
tukio tulishangaa kukuta askali wamejipanga wakiwa na Masiraha mazito mazito na
gafla tulianza kushambuliwa bila kupewa wala kutangaziwa Onyo la aina yeyote
ile, Tulipigwa Risasi za moto na Mabomu na Muheshimiwa alikamatwa kama Jambazi
na kudhalilishwa kisha kusukumwa katika Gari la Police na kupelekwa Kituo kikuu
cha Polisi Nzega Mjini.
Nirudi
kwenye mada ya msingi. Inatokea hivi, hapa na pale katika Jamhuri kwamba
wananchi wanaonewa, serikali ipo na hakuna kuheshimiana miongoni mwa viongozi
wa serikali, Je hii inatokana na nini?
Inakuwaje
kiongozi wa kuteuliwa na asiyewajibika kwa wanannchi anaowaongoza ashindwe
kumheshimu kiongozi wa kuteuliwa mbele ya raia wake bali tu amdhalilishe kuwa
yeye si lolote si chochote? Ama;...
Je...!!
busara ya kukaa mezani na kuzungumza viongozi imetowekea wapi hasa wale wateule
kukaa meza moja na wenye ridhaa ya wananchi? Ama;
Ni
nani aliyewaambia, kwa kuwa Wakuu wa Vituo vya Polisi na Wakuu wa Polisi Wilaya
na Mikoa ni Wateule wa Mteule wa Rais (kwa taathira), na kwa kuwa Rais wa
Jamhuri ana Madaraka makubwa, na kwa kuwa kwa mujibu wa Katiba Rais hawezi
kushtakiwa mahakamani akiwa madarakani, basi na wao wana nguvu hiyo na wana
kinga hiyo? ama......
Ni
nani aliyewadanganya kwamba, kwa kuwa wamepewa Mabomu, Pingu na Risasi, basi ni
lazima vyote vitumike kwa sababu yoyote? Na alafu,
Ni
nani kawaambia kila tukio basi matumizi ya risasi ni muhimu?
Ifike
mahali itoshe na ionekane inatosha maana chuki ni kubwa miongoni mwa viongozi
na wapo wanaojiona kwa vile wao mamlaka yao ya uteuzi ni rais wa jamhuri, basi
na wao ni Marais wa Jamhuri kwa zile nafasi walizoteuliwa kuzishika. Huu ni
Wendawazimu na Ujuha ambao unalitafuna taifa. Taifa hili kwa uchanga wake
kiuchumi linahitaji mshikamano wa hali ya juu kati ya viongozi wa ngazi zote,
kuheshimiana na kuwajibika sawa moja kwa moja kwa wananchi na si kukaa na
kuendekeza ubabe usio na tija.
Tunahitaji
wananchi waone kwamba viongozi wao wanaheshimiana wao kwa wao kwanza,
wanawaheshimu wananchi wanaowaongoza na wanafanya kazi pasipo makinzano. Rushwa
ina tabia ya upofushaji, na ikiwaingia watawala itawapofusha kabisa. Mapambano
kati ya watawala na viongozi yataishia katika watawala kupokea rushwa kwa
wafitini wa uchumi wa wananchi na kisha watawala kutumia nguvu zao zote kinyume
na ubinadamu dhidi ya viongozi na mwisho wa siku kutaibuka machafuko ambayo
hatuwezi kuyatuliza kwa kauli za kitoto. Mapigano ya wakulima na wafugaji
hayaishi, wachimbaji wadogo na wawekezaji hayaishi, dhuluma ya ardhi haikomi,
hili linatokana na watawala kujiona wao ni wakuu wa viongozi maana nafasi zao
hazitegemei miaka baada ya uchaguzi bali ni kazi na taaluma za kudumu.
Naa
haya ni mawazo ya Kijinga.
Peter
Dafi
peterdafi.blogspot.com
No comments:
Post a Comment