Matumizi mabaya ya Vipaji yanaweza kughalimu Taifa. Mbatia
ametumia ujuzi wake wa kuwasilisha mada kupotosha, bunge na Umma na
kutumia Takwimu Vibaya kwa matumizi yake binafsi. Sote tunatumia Takwimu
zilizotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na hakuna nyingine.
Kwa kutumia kipaji chake, Mbatia Kapotosha umma kwa kusema
"Rais Alipotoka kwa Takwimu alizopewa katika kulihutubia Bunge hili Tukufu". Ieleweke kwamba takwimu alizotumia Rais ni takwimu sahihi zilizotolewa na Tume ya Mbadiliko ya Katiba.
Takwimu zilizopo katika hotuba ya Rais zinapatikana katika Ripoti ya Tume Ukurasa 9, 57, 66 na 67. Majedwali
17 (a-f)
yana takwimu husika. Takwimu alizozingumza Mbatia, ndizo hizo
alizozizungumza Rais Kwenye Hotuba yake, Ndizo hizo zilizopo katika
Taarifa ya Tume, Sasa Rais Alipewa Takwimu na Nani?
Alichokifanya Mh. Mbatia ni kujaribu kujikumbusha mahesabu yake
lakini alikuwa ni katika kufurahisha genge kwa kujaribu kuelekeza namna
takwimu zinavyotakiwa kufanyiwa uchanganuzi (
Analysis) hata kama
mahitaji hayakuwa hayo. Kama nia ni kufurahisha Bunge ama kuvutia
usikivu, basi Mbatia atafanikiwa na huo ni Upotoshaji wa Makusudi ambao
mwisho wa siku utaleta mkanganyiko usio na Tija. Mbatia aistumie ujanja
ujanja wa kujenga hoja kwa kupotosha umma akitumia mbinu chafu
kushawishi Bunge liunge mkono hoja yake . Hili Halikubaliki hata kidogo
na ni uvunjaji wa kanuni za Bunge(
Amevunja kanuni 46(e) inayomzuia Mbunge kutumia Majina ya Marais na Waasisi kwa nia ya kushawishi Bunge kumuunga Mkono.
Kwa Kuwa Mbatia ana Kinga ya Bunge maalum ya kutohojiwa chochote,
Namtaka aombe radhi Umma kwa kuweka kumbukumbu sahihi kwamba alichofanya
ni
"Manipulation of Facts Based on Ignorance of Himself and Those who supported him".
Na Hii SI SAWA NA HAIKUBALIKI Mheshimiwa
Paul C. Makonda
Mjumbe: BUNGE MAALUM LA KATIBA
Post a Comment