Wazir
wa Michezo katika Chuo cha Mafunzo ya Uandish wa Habari (DSJ) Mwajuma
Kitwana amefanya ufisadi wa fedha taslimu shilingi laki mbili (200,000)
kwaajili ya nauli ya wachezaji wanaoshiriki katika michuano ya Beach
Socer Higher Learning Institution, michuano iliyoanza siku ya jumapili
ya tarehe 20/4/2014.
Taarifa
za kuaminika ni kwamba Wazir huyo alipokea fedha hizo kutoka TFF
kwaajili ya usafiri wa wachezaji kuelekea katika viwanja vitakavyotumika
katika michuano hiyo inayopigwa mwishoni mwa wiki katika fukwe za
Escape 1 Mikocheni, pamoja na Gorila Beach Kigamboni.
Wakati
timu ya DSJ ikielekea Gorila beach ambapo ndipo ilipocheza mchezo wake
wakwanza dhidi ya NIT, Mwajuma Kitwanda aliwaeleza wachezaji kwamba TFF
haijatoa nauli, hivyo yeye binafsi kama waziri wa michezo na mpenda
michezo akajitolea fedha yake binafsi kutoka ilala hadi kufika Gorila
Beach Kigamboni.
Mara
baada ya timu kufika mtanange dhidi ya NIT ulipigwa, na hadi kipenga
cha mwisho kinapulizwa NIT waliibuka kidedea kwa jumla ya mabao 6 kwa 3
dhidi ya DSJ.
Mara
baada ya mchezo huo ndipo wachezaji wa DSJ walitonwwa na wachezaji
wenzao kuhusu mtonyo uliotolewa na TFF katika stori za hapa na pale.
baadhi ya wachezaji walimuita madam na kumhoji juu ya fedha hizo, ambapo
awali alikana, lakini mara baada ya kubanwa kwa hoja nzito, alikiri
kupewa fedha lakn akasema fedha hizo ni yeye mwenye mamlaka nazo na
hatatoa taarifa yoyote ili juu ya mwenendo mzima wa matumiz ya fedha
hizo.
Mwajuma Kitwana
CHANZO:- DASJOSO
Post a Comment