Home » , » Breaking News:- WABUNGE WA KAMBI PINZANI WASUSIA BUNGE LA BAJETI NA KUTOKA NJE YA BUNGE.

Breaking News:- WABUNGE WA KAMBI PINZANI WASUSIA BUNGE LA BAJETI NA KUTOKA NJE YA BUNGE.

Written By peterdafi.blogspot.com on Friday, May 30, 2014 | 7:52 AM


Mbowe Kiongozi wa Kambi Pinzani Bungeni kashawishi Kambi pinzani watoke na wametoka wote Bungeni.
Lakini wabunge wachache wa Kambi pinzani wanojielewa na uchungu wa Taifa lao wamebakia Bungeni kama Mzee Mlema.
Imekuwa ni Kawaida sasa kwa Kambi Pinza kutoka na kususia Bunge bila kujali hasara waipatayo.

Wadau, hivi sasa Mwenyekiti wa UKAWA na CHADEMA FREEMAN MBOWE anawatangazia wabunge wake kususa bunge hili baada ya kuzisiwa kwa hoja.

Waziri Lukuvi ametoa taarifa kuwa Wabunge wa UKAWA walikutana leo mchana na kujadili hali ya mjadala wa Wizara ya Nishati na Madini. Katika Mkutano huo, wamekubaliana kuwa wasusie Bunge kwa kuhofia majibu ya Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Mhongo. Amesema kuwa UKAWA wanajua kuwa hoja walizowasilisha ni nyepesi na kwamba Waziri Mhongo atazijibu kwa weledi mkubwa hali itakayoaibisha kambi hiyo. Hivyo ili wasuvuliwe nguo hadharani, ni bira wakasusa kwa hoja ambazo hazina mashiko



 
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger