Mwenyekiti wa baraza la maimam na muhubiri maarufu nchini Kenya Sheikh Mohammed Idris, ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Mombasa karibu na msikiti ulio karibu na nyumbani kwake eneo la Likon baada ya kuvamiwa na kundi la watu waliokuwa na silaha, wakati akitoka nyumbani kuelekea msikitini.
Taarifa kutoka katika eneo hilo zinasema kuwa Sheikh Mohammed Idris alikuwa akipata vitisho vya mara kwa mara kutoka kwa kundi la vijana wa kiisilamu wanaodai mabadiliko, na amewahi kutoa taarifa za vitisho hivyo na kusema kuwa anahofia maisha yake.
Decemba mwaka jana Sheikh Idris na mpinzani wake Mohamed Khalifa
walinusurika kifo baada ya msikiti wao kuvamiwa na vijana zaidi ya 100,
ambao walitawanywa na polisi.
Mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya kumbukumbu ya Pandya, mjini Mombasa.
Bado watazidi kuuwana wenyewe kwa wenyewe mpaka lini?, Tubadilishe Fikra zetu kisha tumuogope Mungu na Tupendane Wanadamu.
#OneLove
#OneHeart

Post a Comment