TANZIA:
Mnamo 11/06/14 majira ya 01:00hrs huko kituo kidogo cha Kimanzichana
Pwani,
watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema waliingia kituo
kidogo cha Polisi Kimanzi Chana huku wakikimbia wakiwa na silaha za
jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu wanaohitaji msaada.
Cha kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye silaha ambaye
amefahamika kwa jina la JOSEPH NGONYANI na kuanza kumkatakata mapanga na
hatimaye kupora silaha SMG ikiwa na risasi 30. Ndipo walipoanza
kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya pili
na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41 na kutoweka
kusikojulikana. Askari Ngonyani alifariki dunia alipokuwa anapatiwa
matibabu kwenye hospitali wilaya ya Mkuranga. Askari mwingine aitwaye
VENANCE amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo bado imo ndani, na kwenye
paja la mguu wa kulia. Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na
kuvimba bega kutokana na kupigwa sana mateke na kujeruhiwa mbavuni. Kwa
mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo aitwaye VERONICA MUSIME,
anathibitisha askari huyo kufariki akiwa anapatiwa matibabu hapo
Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili kwa matibabu ya kina.
Kazi ya Mungu haina makosa; vituoni tuwe makini sana na stahili hii ya
ujambazi; HESHIMA PEKEE kwa marehemu na majeruhi hawa ni kuwapata
watuhumiwa wote na silaha walizoiba bila kuchelewa. Bila kujali mkoa
ulipo, taarifa za haraka tunatarajia kupata toka kwako kuhusiana na
wahusika wa tukio hili. AMEN
Post a Comment