Home » , » WASIOJULIKANA WAITEKA A/C YA MBUNGE DK. HAMISI KIGWANGALLA

WASIOJULIKANA WAITEKA A/C YA MBUNGE DK. HAMISI KIGWANGALLA

Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, June 10, 2014 | 1:18 PM


 Dk. Hamisi Kigwangalla alisema haya Jana kupitia Account yake ya FB kuwa kuna watu wameHack A/C ya FB na Kuanza kupost Mambo ya Ajambu Soma Hii alosema HK......


"Napenda kutoa taarifa kuwa account yangu ya Facebook kwa siku mbili sasa imekuwa ikichezewa, imetekwa nyara (hijacked) na watu wasiojulikana, na wamekuwa wakiitumia kuwadanganya wananchi kuwa ninatoa mikopo kwa masharti fulani nafuu, na pia kuwa nimetumwa na Katibu wa Bunge nitafute mkandarasi wa mambo ya TEHAMA (IT) ama kuwa nahitaji teknolojia ya malipo kama ya tiGopesa (bulk money payment). Taarifa hizi si za kweli. Naomba kwa ujumbe huu umma utambue hili na ninatoa wito kwa umma kuwa makini na taarifa zozote zitakazohusu mambo ya pesa ama mengine yoyote yale yanayotia shaka kama haya ama yasiyoendana na mwenendo wa kawaida wa matumizi yangu ya account hii ya facebook. Tafuta namna ya kuhakiki kila taarifa mtakazozipata zikielezwa zinatoka kwangu. Timu ya wataalamu wa cyber crimes wanafanya kazi kuwafuatilia na kuwabaini watu hawa ili wachukuliwe hatua stahiki."

Watu wengi wamekuwa wakilalamika kwa hili A/C zao za Mitandaoni kuhujumiwa na watu wasiojulukana na kupost mambo ya Ajabu.
Kuwa makini sana wewe Mtumiaji wa Mitandaoni.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger