Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahamani Kinana akiongozwa na Mkuu wa
Moa wa Singida Dk, Parseko Kone, Katibu Tawala Lianna Hassan na
viongozi wengine wa Mkoa wa Singida kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi
wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, wakati Kinana alipokuwa Mkoani
Singida kwa ziara ya kikazi ya siku saba.(Picha na Zainul Mzige wa
modewjiblog).
Na Nathaniel Limu, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone amesema serikali
imetoa zaidi ya shilingi 6.7 bilioni kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa
hospitali ya rufaa ya mkoani hapa iliyoko kijiji cha Madewa nje kidogo
ya Singida mjini.
Dk.Kone amesema hospitali hiyo itakapokamilika,itahudumia wagonjwa kutoka mikoa yote ya kanda ya kati.
Mkuu huyo alitoa rai hiyo wakati akitoa akitoa taarifa yake kwa
katibu mkuu CCM taifa,Abrahamani Kinana aliyetembelea hospitali hiyo
hivi karibuni.
Amesema mkoa umetegewa eneo la ekari 283 kwa ajili ya uendelezaji
wa mradi wa hospitali hiyo, ambayo itakuwa ya mfano hapa nchini.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Dorothy Gwajima
amesema lengo la mradi huo ni kuimarisha huduma za afya mkoani pamoja na
mikoa jirani.
Katibu Mkuu wa CCM akiweka saini kwenye kitabu cha
hospitali ya Rufaa huku Naibu Katibu Mkuu wake Mwigulu Nchemba na mkuu
wa Mkoa wa Singida Kone wakishuhudia.
Dk.Gwajima amesema mradi huo utakapomalizika,utakuwa na majengo 29 yatakayotumika kutoa huduma mbali mbali.
Mganga huyo mkuu,amesema changamoto inayowakabili ni pamoja na
uhaba wa watumishi,nyumba za kuishi watumishi na ufinyu mdogo wa bajeti
ya dawa kutoka bohari kuu ya madawa (MSD).
Kwa upande wake Kinana,alitumia fursa hiyo kumpongeza Dk.Kone kwa
utendaji kazi wake ambao umesaidia kujengwa kwa hospitali hiyo.
Mganga mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Singida (RMO) Bi. Doroth Gwajima akisoma taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo.
Amesema baada ya mradi huo kukamilika mkoa wa Singida utaondokana na matatizo ya huduma za afya.
“Ili kumuunga mkono Dk.Kone kwa hili jambo nzuri la ujenzi wa
hospitali ya rufaa ambayo itasaidia Watanzania wengi kupata huduma ya
afya kwa kiwango kizuri,nitahakikisha nina muunganisha na baadhi ya
marafiki zangu wa ndani na nje ya nchi ili waweze kusaidia kumalizika
kwa ujenzi wa hospaitali hii inayovutia”,amesema Kinana.
Mganga mfwawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, Dkt
Joseph Malunda, akiwaonesha michoro ya hospitali hiyo viongozi
walioambatana na Kinana.
Viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakimsikiliza Dkt Malunda.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Pendael Maasai akisisitiza jambo kwa Kinana.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Pendael
Maasai akimwonyesha Katibu Mkuu kinana vifaa mbalimbali vilivyopo kwenye
hospitali hiyo ya rufaa.
Mbunge MO akiangalia mojawapo ya vifaa vya hospitali ya rufaa ya singida.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mohammed Dewji akisalimiana na
Daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama wa mkoa wa Singida Dkt, Seleman
Mutani wakati wa ukaguzi wa hospitali hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa akiongozana na mkuu wa Mkoa Kone, Mbunge
wa jimbo la Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji, wasaidizi wa Mbunge Duda
Mugheny na David Mkufya wakimwongoza Kinana kutoka nje mara baada ya
kukagua hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo.
Post a Comment