Picha zikionyesha matukio mbalimbali kabla wakati na baada ya Mhe. Dr Hamis Kigwangalla mbunge wa jimbo la nzega kwa tiketi ya chama cha mapinduzi kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwakani kupitia chama cha mapinduzi ccm endapo kitampa ridhaa ya kupeperusha bendera ya ccm kwenye kuwania urais ,akizungumza mbele ya waandishi wa habari asubuhi ya leo Dr kigwangalla alisema ameamua kutangaza nia ya kuwania urais kwa maono yake mwenyewe kwa mapenzi mema kwa taifa la tanzania na sio kwa kushinikizwa na mtu yoyote nje au ndani ya chama chake,aidha alieleza kuwa nia yake ni kujenga Tanzania yenye uchumi uliotengamaa ukilinganisha na kwa sasa ambapo uchumi wa nchi haukuwi kulinganisha na maliasili za nchi zilizopo hazitumiki kuimalisha uchumi wa nchi na kujenga taifa lisilo na matumaini huku wananchi wakikosa huduma muhimu kama maji chakula huduma ya afya pamoja na miundombinu ya uhakika.alisema endapo atapewa nafasi hiyo atajenga Tanzania yenye uchumi imara yenye utawala bora pamoja na kuheshimu utu wa mtanzani ambao kwa sasa umepoteza thamani yake .Dr kigwangwalla anakua kijana wa kwanza wa kitanzania ambaye alizaliwa tarehe saba mwezi wa nane mwaka 1975 kutangaza nia ya kuwania urais hadharani bila woga, huku akijiamini kwa kiasi kikubwa akijibu moja ya maswali ya waandishi wa ha habari kuhusiana kulitetea jimbo la nzega Dr kigwangwalla alisema nitaacha kutetea jimbo la nzega endapo chama kitanipa ridhaa ya kuwania urais lakini kama chama hakitanipa ridhaa ya kuwania urais kupitia chama changu nitagombea na kutetea jimbo la nzega kwa nguvu zangu zote.
Post a Comment