Home » , » Mwenyekiti TCD na UDP John Monose Cheyo Asema Mchakato wa BMK unaendelea Vema

Mwenyekiti TCD na UDP John Monose Cheyo Asema Mchakato wa BMK unaendelea Vema

Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, September 11, 2014 | 10:28 PM

Akitoa mchango wake kwenye Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa TCD na UDP John Momose Cheyo anasema kuwa mchakato wa bunge unaendelea vema. Alisema kuwa wakati walipozungumza na Rais Kikwete, wajumbe wa TCD walikubaliana kuwa Bunge liendelee mpaka likamilishe kazi ya kutunga katiba inayopendekezwa. Kwamba wamekubaliana kuwa Bunge Maalum likamilishe kazi yake na ana imani kuwa kazi hiyo itakamilika. Anasema kuwa bunge hili haliendeshwi kwa kelele za barabarani bali linaendeshwa kwa sheria. Alitaja sheria hiyo kuwa ni GN 254 ambayo inataja uhai wa bunge hili kuwa unaishia tarehe 5 Oktoba 2014. Amempongeza Rais Kikwete kwa kuwa mfano wa kuigwa katika kuleta suluhu ya jambo hili.

Amesema kuwa kila mtu amerekodiwa jinsi alivyoongea wakati wa majadiliano hivyo ameomba zitengenezwe CD na kuzisambaza ili Watanzania wajue nini viongozi wao waliongea. Anawashangaa sana ukawa kwa kupiga kelele barabarani ilhali wakiwa na Rais hawakuongea wanayoongea mtaani. Anasema kuwa yale waliyoongea mbele ya waandishi wa habari ndiyo waliyokubaliana wakati wa mazungumzo. Anasema kuwa bunge hili lina watu makini na amewataka wabunge wajiamini ili wakamilishe kazi zao kwa wakati.

Anasema kuwa kuna mambo mengi mazuri yamezungumzwa kwenye bunge maalum hasa juu ya mambo yanayowahusu watanzania. Ametaja mambo hayo kuwa ni yale yanayowahusu wakulima, wafugaji, wavuvi nk. Pia amesema kuwa suala la muungano limepatiwa ufumbuzi. Kwamba Rais wa Zanzibar atakuwa makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu atakuwa Makamu wa Pili wa Serikali ya Muungano.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger