POLENI SANA WAANDISHI MLIOCHAPWA NA ASKARI
Maoni yangu kwa Waandishi
Ndugu watanzania wenzangu naomba nianze kwa kuwapa pole wale wotewaliofikwa na matatizo ya kuchapwa na Askari pale Makao makuu ya Jeshi la Polisi.
Nawapa Pole sana waandishi wenzangu wale waliopatwa na Matatizo ya Kuadhibiwa na Askari pale walipokuwa wakiangaika kupata habari. Hakika inauma na Kusikitisha sana pale unapokuwa umedhamilia kufanya kazi yako Kwa ufasaha na uweledi, lakini kinatokea kikwazo na kinakuwa kigumu zaidi hata kufikia kuumia, hii inasikitisha sana. Hivo poleni sana wale wote waliofikwa na Matatizo hayo.
Lakini napenda kuchukua nafasi hii pia kusema kuwa Waandishi wa Habari tumekuwa tukifanya kazi kwa Mazoea, tena tunafanya kazi katika sehemu hatarishi bila kufahamu sisi ni waandishi na tunaamini kuwa kazi yetu itatulinda kama waandishi na hata kufikia kuvunja, kutokufuata, kuzembea, kupuuzia Utaratibu ama kuona watanifanya nini mimi Mwandishi.
Jana pale Makao Makuu ya Polisi palikuwa na sintofahamu kwakuwa Askari wote waliokuwapo pale walikuwa Kazini na walienda wakiwa hawaitaji undugu wala kujuana kwa maana yakwamba, Jambo ama Tamko lililompelekea Mbowe kuitwa Kuhojiwa halikuwa tamko la kawaida ni Tamko Hatarishi na Lenye Mlengo Hasi kitaifa, jambo ambalo wao kama Askari linawapa wakati mgumu sana kwani itawalazimu waishi maisha yakutokuwa na amani na kufanya kazi ngumu sana yakuwalinda Raia wote na Mali zao katika mazingira hatarishi ya Maandamano bila Kikomo,bila Kibali wala Kizuizi, popote Maandamano yatakapoelekea basi wao walinde Mali na wenyemali hizo Tanzania Nzima.
Ivo sasa kutokana na hayo Askari anapaswa kufanya kazi yake aliyoisomea darasani na kuifanyia mazoezi (DEPO) kwa muda wote huo.
Linapotoka Tamko na Amri ya KIJESHI/PILISI Mtu yoyote mbele ya Askari ambae haeleweki wala kusomeka vema huwa ni chakula cha askari. kwani Askari yuko pale katika eneo la tukio Kazini kama wewe Mwandishi kazini, na unapokuwa kazini kila ukionacho unaandika kama kinahusiana na Tukio husika. Jana ilitoka Amri ya kutawanyika na watu wakaendelea kushangaa eneo la tukio, kwa bahati mbaya palikuwa na wananchi ndani ya wafuasi wa CHADEMA wakiwa wamechanganyika. Tukumbuke askari pia nibinadamu akichelewa kukushulkia wewe utamshulkia, tumeona haya mara nyingi sana Nchini na hata Nchi za wenzetu. Ivo Unaposikia Utaratibu wa kazi ya mtu lazima uheshimu na ufuate, ukiwa kama mwandishi wa habari unapaswa kuwa wakwanza kwa nidhamu ili hata habari uandikayo iwe imejaa HEKIMA na BUSARA
Nakumbuka wakati nasoma tulisoma MEDIA ETHICS hii misingi tunapaswa kuifuata sana ili kutupa Dira ya kazi na Mpangilio sahihi wa kazi zetu bila kutizama tunamwandikia nani wapi na kwanini.
KITAMBULISHO
Kitambulishi ni Muhimu sana kwa Mwandishi, tena sio tu Kitambulisho kwa mana ya ID Card hapana, Mwandishi unapaswa kuwa na Vazi maalumu linalokutambulisha wewe kama mwandishi hata kama uko mita mia moja nikikuona bila ya ID nijue wewe ni mwandishi wa habari tena hata nijue unatoka chombo Fulani. Kwa maana ya kuvaa Kofia pia Kikoti cha mifuko mifuko na vyote vikiwa na nembo ya ofisi yako, Dunia Nzima waandishi wanafanya hivo hasa wanapokuwa katika shuguli ngumu kama hiyo ya jana ambayo inahusisha unuvunjifu wa amani kwa tishio la maandamano NK…..
Hivo waandishi Wenzangu nawaomba na kuomba tena na tena tuipende kazi yetu na tuifuate misingi na taratibu za kazi zetu, pia tuheshimu kazi za wenzetu kwani nao wako kazini kama sisi tunapokuwa kazini vile vile.
Mimi nimewai Kukamatwa nakushitakiwa kuwa nimiongoni mwa waandamanaji, na kweli nilikuwapo katika kusanyiko hilo siwezin kukataa, CAMERA na Kila kitu nilikuwa nacho lakini Sikuweza kuonyesha kitambulisho kwa wakati, Askari wakanikamata na kuniweka Lumande kwa zaidi ya masaa 5, Niliwalaumu na kuwalaani sana, lakininilitafakari sana baadae nikagundua ilikuwa ni haki yao wao kama askari kufanya kila wanachohisi hakiko sawa kwa maana ya kulinda mali na lasilimali za watu, kama kuna wanaemshuku nilazima wamkamate na kumchukua maelezo, na unapokataa kutii sharia bila Shuruti basi niwajibu wao kukushurutisha kama mafunzo yao yasemavyo.
CAMERA sio kitambulisho tosha kutoa majibu kuwa wewe ni mwandishi kwani Dunia ya Leo kila mmoja ana CAMERA, Ivo tuzingatie kuwa wawazi na kufuata utaratibu wa Kazi, Kitambulisho, Vazi maalumu na Kofia.
Ili tuwe wamoja na kujenga taifa moja lenye Amani na Upendo tunapaswa kuwa na NIDHAMU kwa kila jambo tulifanyalo.
Ili tufanye kazi zetu vema Lazima tuning’inize Kitambulisho shingoni pia kuvaa kikoti na kikofia cha utambulisho kwa mtu yeyote akikuona ajue wewe ni Askari.
Mwisho Askari nawaomba pia tuwe makaini na kila jambo tulifanyalo, ingawa askari huwa wachache kuliko waandamanaji ivo lazima mtumie nguvu ili kuhakikisha hamzidiwi, ila tufanye kazi kwa uweledi wakutosha ili kuepusha migogoro kama hii kwa watanzania ambao ni ndugu site.
TANZANIA NCHI YETU WATANZANIA, TUTAIJENGA AMA KUIBOMOA SISI WENYEWE WATANZANIA, NA TUKUMBUKE TUKIIBOMOA KWA KUSABABISHA VITA MA MACHAFUKO WATAKAO UMIA NI MIMI NA WEWE KINA KAJAMBA NANI HAO KINA MBOWE NA KINANA MAKATIBU WA VYAMA WATAPANDA NDEGE NA KUHIFADHIWA MAHALA SALAMA, MIMI NA WEWE PIA MAMA NA WADOGO ZETU NDIO WAANDISHI WA BBC WALIOVALIA VIKOTI WATAKUWA WAKIRIPOTI VIFO VYETU AU UKIMBIZI WETU NCHI ZA JIRANI.
MWANDISHI TUMIA KARAMU YAKO KUELIMISHA WATANZANIA KWA KUWALISHA UKWELI BILA KUPENDELEA WALA KUTIA HASIRA HATA KUJENGA CHUKI KWA TAASISI WALA MTU FULANI.(MEDIA ETHICS)
Mungu Ibarariki Tanzania.
Ni Mimi Kijana Mtanzania Mzalendo Mpenda amani na Upendo kwa Watnzania wote bila Itikadi wala Dini zetu.
Peter Dafi
Post a Comment