MAFURIKO
Mvua kubwa iliyonyesha mjini Morogoro jana kwa muda mfupi tu
ilisababisha mafuriko katika baadhi ya barabara za mji kiasi cha
baadhi ya barabara kushindwa kupitika kutokana na kufurika maji.
Maji hayo yaliingia hadi ndani ya baadhi ya maduka na kuleta kero
na hata hasara kwa wafanyabiashara hao.
Wakazi wa mji wa Morogoro wakizungumzia mafuriko hayo
wameilalamikia miundombinu mibovu ya barabara kutokana na
kuziba kwa mitaro ambapo wameitaka halmasauri ya mji wa
Morogoro kuzibua mitaro hiyo huku baadhi ya wafanyabiashara
wakilalamika kupata hasara.
Katika hatua nyingine mto Kikundi uliopo mjini Morogoro umepoteza
uelekeo na kumwaga maji katika soko kuu la mji wa Morogoro na
kusababisha maji kujaa katika maduka huku baadhi ya magari
yakiingia kwenye mitaro na baadhi ya bodaboda zikiwa na abiria
kuzama katika maji na kulazimika kuvutwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Phimlemon Magesa
akizungumzia malalamiko hayo ya wananchi hao amesema manispaa
wanajitahidi kufanya usafi lakini tatizo liko kwa wananchi wenyewe
kwani hutupa taka kwenye mitaro na kusabisha kuziba na maji
kupoteza ueleko na kujaa katika makazi ya watu.MOROGORO
Soko Kuu la Morogoro likiwa limezingirwa na maji jana baada ya mvua kubwa
kunyesha na kusababisha mafuriko katikati ya mji kutokana na mto Kikundi kujaa
mchanga.
Picha na Juma Mtanda
Post a Comment