Home » , » Hotuba ya Mh Bernard Membe aliyoitoa Kanisa la Anglikana Jana.

Hotuba ya Mh Bernard Membe aliyoitoa Kanisa la Anglikana Jana.

Written By peterdafi.blogspot.com on Sunday, January 4, 2015 | 9:17 PM

*HOTUBA YA MHESHIMIWA BERNARD K.MEMBE,
WAZIRI WA*
*MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
KWENYE*
*MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA KANISA ANGLIKANA,
*
*DAYOSISI YA DAR ES SALAAM, TAREHE 4 JANUARI,
2015*
*Mhashamu Baba Askofu Dr.Valentine Mokiwa, Askofu
wa Dayosisi ya*
*Dar es Salaam;*
*Kasisi Mkuu Kiongozi Canon John Mlekano;*
*Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Dar es salaam- Canon
John Senyagwa,*
*Wakuu wa Majimbo mliopo hapa,*
*Ndugu waumini; *
*Wageni waalikwa;*
*Mabibi na Mabwana;*
*Bwana Asifiwe....!*
*Shukrani kwa Mwaliko*
Nakushukuru sana Baba Askofu Mokiwa, viongozi
wenzako pamoja
na waumini wote wa Dayosisi ya Dar es Salaam kwa
kunialika kuja
kushiriki nanyi katika maadhimisho haya ya kihistoria
ya Jubilei ya Miaka
Hamsini ya Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar Es
Salaam.
Nawapongeza sana waumini wa Dayosisi ya Dar es
Salaam kwa ku-
timiza nusu karne tangu ianzishwe. Miaka hamsini si
haba, ni umri wa
makamo, na kwa kipimo chochote kile ni umri mrefu.
Umri huu ni kipimo
cha ukomavu wa Dayosisi ya Dar es Salaam. Ni miaka
50 ya uinjilisti, up-
onyaji na huduma kwa jamii. Mafanikio haya ya
Dayosisi ni kielelezo cha
uimara wa Kanisa la Anglikana. Hatuna shaka kuwa
mmeweza kudumu
kwa muda huo kutokana na misingi imara ya kiroho na
uongozi uliojeng-
wa juu ya miamba iliyowatangulia. Hatuwezi
kuzungumzia mafanikio ya
Dayosisi hii bila kumtaja Baba Askofu John Sepeku na
wenzake waliolijen-
ga Kanisa hili.
Kanisa la Kianglikana la Tanzania ni miongoni mwa
majimbo mawili
tu ya kianglikana duniani kuwa na muungano wa
mapokeo mawili ya
kanisa Anglikana - yaani High Church (lililokuwa na
mrengo wa kikatoli-
ki) na Low Church (lililokuwa na mrengo wa kiinjili).
Kanisa la Kiang-
likana la Tanzania na lile la Burma pekee ndio
yaliyoweza kuunganisha
mapokeo haya mawili na hatimaye kuwa na kitabu cha
sala kimoja, litru-
gia moja, na uongozi mmoja wa Askofu Mkuu ambao
unasomwa katika
parokia zote. Ndio maana haishangazi kuwa kanisa
Anglikana la Tanzania
lilisimama imara bila hofu kupinga ndoa za jinsia moja
hata pale makanisa
mengine ya Anglikana duniani yalipoamua kufanya
hivyo. Mlinipa faraja
kubwa, maana kupitia kwenu ile sauti ya Serikali, na
sauti ya watanzania
kukataa shinikizo kutoka nje ya nchi la kukubali ndoa
za jinsia moja lilipa-
ta nguvu na mwangwi mkubwa. Mlinitia nguvu sana
pale niliposimama
kidete kuwaambia rafiki zetu wa nje kuwa katika hilo
la ndoa za jinsia
moja, Tanzania tunaomba tukubaliane
kutokukubaliana.
Tunapojitokeza kwa kutimiza miaka 50 ya Dayosisi ya
Dar es
Salaam , hatuna budi kukumbushana kuwa safari bado
ni ndefu. Tulipoto-
ka kweli ni mbali, tunapokwenda ni mbali zaidi. Ipo
zaidi ya miaka 50

mingine mbele ya Kanisa hili. Hivyo leo tunaianza
safari mpya, katika
mwaka mpya na matumaini mapya. Sisi katika Serikali
tunayo matumaini
makubwa na safari yenu. Katika miaka 50 ya uhai wa
Dayosisi,
Tumeshuhudia kazi zenu na huduma zenu. Siku zote
mmeshirikiana na
Serikali katika kutoa huduma za jamii na kuilea amani
yetu.
Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea
kushirikiana na
Kanisa la Anglikana pamoja na madhehebu mengine ya
dini kuboresha
maisha ya Watanzania. Tutaendelea kupokea ushauri
wenu na kuwashirik-
isha katika mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo
ya nchi yetu na
watu wake. Naomba muendelee kushirikiana na
Serikali katika kutoa
huduma kwa wananchi. Muendelee kutumia mtandao
wenu mpana uliopo
nchi nzima kwa ustawi na maendeleo ya nchi yetu.
Lengo letu libaki kuwa
moja daima na milele.
*Maombi kwa Viongozi wa Dini*
*Mhashamu Baba Askofu Dr. Mokiwa,*
*viongozi wa dini mliopo;*
*Mabibi na Mabwana;*
Mwaka huu wa 2015 ni mwaka wa kipekee sio tu kwa
Kanisa lenu
linaloadhimisha miaka 50 ya Dayosisi ya Dar es Salaam,
bali pia kwa
watanzania wote. Mwaka huu una mambo makubwa
mawili yaliyo mbele
yetu yaani kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa
na uchaguzi mkuu
wa Rais, Wabunge na Madiwani. Kama ilivyo kwa
Dayosisi yenu, Taifa
letu nalo linaianza safari ya miaka 50 ijayo na kufika
kwetu huko ku-
tategemea na jinsi tunavyoianza safari yenyewe.

Nchi yetu inapita katika kipindi cha majaribu
makubwa na mitihani
mikubwa. Tunalo tatizo la mmomonyoko wa maadili
katika ngazi zote
kuanzia familia, shule, ofisi na serikalini. Tunalo tatizo
la ufisadi,
ukatili
dhidi ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi,
na tunalo pia tatizo
la umasikini. Tunalo tatizo la kupoteza uvumilivu wa
kidini na kisiasa.
Watanzania wengi wamefika mahala wanaanza kukata
tamaa na kupoteza
matumaini. Changamoto hizi zinawasumbua pia
viongozi wa dini zetu
zote. Waumini wamekata tamaa na kupoteza hofu ya
Mungu. Kumekuwe-
po na wengi sasa wanaokimbilia kwenye nguvu za giza,
uganga na una-
jimu. Tunahitaji kutoka hapa. Tunajiuliza wote,
tunatokaje?
*Baba Askofu Dr. Mokiwa;*
*Ndugu zangu;*
Habari njema ni kuwa, nyakati za majaribu hazidumu.
Mashaka na
majaribu humfika mwanadamu ili kumuimarisha kila
anapoukaribia
mwisho mwema. Majaribu ni kipimo cha imani.
Tunaletewa majaribu ili
tuyashinde sio tuyakimbie. Tunayo fursa muhimu
mbele yetu, kura ya
maoni ya Katiba Inayopendekezwa na muhimu zaidi
Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba 2015. Sote tumefuatilia kwa makini mchakato
wa Katiba na
tumeshiriki kwa hatua mbalimbali. Tumebakiza hatua
moja muhimu, nayo
ni kupiga kura ya maoni tarehe 30 Aprili, 2015. Sote
tujiandae kuipigia
kura na sote tutoke tukafanye uamuzi sahihi.
Fursa nyingine muhimu ni uchaguzi mkuu wa Oktoba
2015. Uch-
aguzi wa mwaka huu ni muhimu sana kwani
tunachagua Rais mpya
atakayeunda Serikali mpya ya awamu ya tano. Rais wa
awamu ya tano
atategemewa kuendeleza mema ya awamu ya nne na
awamu zilizopita, na
kutoa majawabu kwa changamoto za sasa na zijazo na
kutusogeza karibu
zaidi na Tanzania njema tunayoitamani, Tanzania
yenye neema tele.
Hatuko mbali na nchi yetu hiyo ya ahadi. Serikali ya
awamu ya nne imefanya mengi sana makubwa ya kujenga misingi ya kutufikisha huko.
Tumepanua nafasi za elimu, afya na huduma za jamii,
tumejenga miun-
dombinu ya kutuwezesha kufika huko, uchumi
umekuwa sana lakini
umasikini haujapungua kulingana na kasi ya kukua
kwa uchumi. Bahati
nzuri tunazo rasilimali zinazoweza kutuvusha katika
hatua hii ya mwisho
kuifikia neema mbele yetu.
Wengine wetu tumejiuliza sana, nini basi kinasimama
kati yetu na
neema iliyo mbele yetu ikiwa uchumi unakua na
tumewekeza katika mi-
undombinu muhimu na rasilimali tunazo? Yako
majawabu mengi tofauti.
Jawabu moja ambalo linasemwa na kukubalika na
wengi ni kuwa,kina-
chosimama mbele yetu, na kati ya umasikini wetu na
neema iliyo mbele
yetu ni rushwa na ufisadi. Wako wanaotoboa mtumbwi
wetu tunaosafiria
pamoja na jitihada zetu za kupiga makasia.
Mimi sipendi rushwa na ufisadi. Nashukuru Mungu
kuwa rushwa,
ufisadi na mafisadi hawanipendi zaidi. Siwaonei wivu
wale wanaopend-
waa mafisadi, natosheka kupendwa na wale wenye
mapenzi mema na taifa
letu. Jukumu la kuzuia ufisadi ni la kila mmoja wetu
katika kila eneo lake
na kwa nafasi yake. Sio jukumu la viongozi pekee, au
chama fulani pekee,
maana mafisadi wako kote katika ngazi zote. Naamini,
mwaka huu, wengi
wetu tukisema hivyo, tukasimama katika mstari huo, na
tukaenenda
hivyo, ufisadi hauwezi kutushinda. Kila mmoja na
asipuuze udogo wa
sauti yake,au uchache wetu dhidi ya wale waovu,
maana hata mwale
mdogo wa mshumaa hufukuza giza.
*Baba Askofu,*
Kwa kuwa uchaguzi kwa nchi yeyote ile ni jambo
kubwa, naomba
Kanisa na waumini kwa ujumla waliombee taifa letu ili
Mwenyezi Mungu
atuongoze kuchagua viongozi wenye uwezo, busara na
hekima ya kutatua
changamoto zinazolikabili taifa. Tuchague viongozi
waadilifu, wazalendo,
wachapa kazi, wasio na uchu wa madaraka kwa ajili ya
kujinufaisha wao
binafsi na marafiki zao.
*N*inawasihi viongozi wa dini muongeze juhudi za
kuhubiri umoja
na kutoa mafundisho ya kuhimiza udugu na
mshikamano miongoni mwa
waumini na watanzania kwa ujumla. Watu wapendane
na washirikiane
bila kujali itikadi za vyama vyao au ushabiki walionao
kwa wagombea.
Tukumbushane kuwa chaguzi zinakuja na kuondoka
lakini amani
yetu, usalama wetu, udugu wetu na umoja wetu ndio
nguzo kuu za uwepo
wa taifa letu. Tusikubali kupoteza kwa gharama yeyote
tunu hii ya amani,
mshikamano na umoja wetu. Amani ya nchi yetu
ikitoweka, umoja na
mshikamano wetu ukivunjika, hakuna atakayesalimika
itaathiri wote
waliokuwamo na wasiokuwamo. Hivyo tunao wajibu
wa kuidumisha
amani. Nasema hivyo kwa sababu nimeyaona
mwenyewe kwa majirani
zetu.
*Mhashamu Baba Askofu;*
Ombi langu lingine kwenu - tuendelee kusaidiana
kuilea nchi yetu
kiroho na kimaadili. Sisi tutaendelea kuhangaika na
afya za miili na akili
za
watu wetu. Tutaendelea kuwekeza katika afya,elimu na
huduma za jamii.
Jitihada hizi za serikali ni kazi bure ikiwa dini zetu
zote nchini haz-
itawekeza kwenye afya ya mioyo ya watu wetu. Maana
binadamu hakami-
liki bila afya ya roho.
Mimi naamini kwa dhati kuwa watu wakishika
mafundisho ya
dini, wakamuogopa Mwenyezi Mungu, maovu mengi
yatapungua.
Hayawezi kuisha kabisa lakini yatapungua sana. Ninyi
viongozi wa dini
mnayo nafasi ya pekee kwa vile mnasikilizwa sana na
waumini wenu. Ma-
neno yenu yanapokelewa vizuri kuliko wanasiasa au
watu wengine.
Hivyo, tusaidiane kulea taifa letu ili lisiangamie. Hebu
kila mmoja alime
mrsba wake. Najua ni kazi ngumu hususan katika
kipindi hiki cha utan-
dawazi lakini tusichoke. Tuweke mkazo zaidi kwa
vijana kwa sababu wao
ndio wahanga wakubwa lakini pia wao ndio taifa la leo
na kesho, ndio
warithi wa taifa letu. Tukiwaandaa vyema, mustakabali
wa taifa letu na
watu wake utakuwa kwenye mikono salama.
Tukishindwa leo, tutalia na
kusaga meno kesho. Taifa letu litakuwa mashakani.
*Mwisho*
*Mhashamu Baba Askofu Dr. Mokiwa* *;*
*Viongozi wa Kanisa la Anglikana* *;*
*Ndugu waumini* *;*
*Mabibi na Mabwana* *;*
Nimesema mengi, lakini nilidhani ni vizuri nikayaeleza
hayo niliy-
oyaeleza kutokana na mazingira na nyakati zenyewe
wakati tukishere-
hekea miaka 50 ya kanisa hili na tukizitazama nyakati
muhimu kwa kanisa
na taifa zilizo mbele yetu. Nakushukuru kwa mara
nyingine tena
Mhashamu Baba Askofu kwa uongozi wenu imara
ambao umeliwezesha
kanisa katika kupata mafanikio makubwa sana katika
miaka 50. Naomba
Mwenyezi Mungu awaongezee neema na karama ili
kupata mafanikio zai-
di siku za usoni . Mimi nitakuwa nanyi bega kwa bega
katika safari ya
kanisa hili huko mbele tuendako, kama nifanyavyo
kwa makanisa na dini
nyingine kwa kuamini kuwa sote tunafanya kazi ya
Mungu mmoja.
Naomba tuendelee kushirikiana kuleta maendeleo zaidi
kwenye Dayosisi
yenu na nchi yetu kwa ujumla. Tukiunganisha nguvu
zetu, daima ushindi
utapatikana. Basi tuamue sasa kuwa washindi.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger