Salma Said wa Gazeti la Mwananchi.
Nimefadhaika na kushangaa kwa taarifa yako uliyoitoa kwenye gazeti lako la MWANANCHI la tarehe 17 Januari 2016 uk wa 3 yenye kichwa cha habari MGONGANO MPYA WA KISHERIA UCHAGUZI ZANZIBAR WAIBUKA.
Bi Salma tunakushangaa sana kwa kushabikia CUF hadi unakuwa kipofu. Kwanza napenda nikueleze kwamba maadili ya uandishi huna si leo wala si jana. taarufa zako zote ni za uchonganishi na uzandiki na zilizojaa mahaba ya ucuf. Sijui huu utaalamu wako ukoje wa uandishi. kwa ufupi huwafanyii haki wananchi wa Zanzibar na Tanzania. Habari zako ni za kupotosha jamii kisiasa na za kumjenga unaempugia debe Seif Sharif.
ushahidi wa hayo ni huu upuuzi wako uliouandika leo kwenye gazeti la mwananchi. Unaelezea kwamba fedha za uchaguzi zimeidhinishwa na nani???
Nikuulize maswali yangu Bi Salma halafu unijibu ukipata wasaa.
1. Kwenye taarifa yako kwanini hukuelezea au kutamka kwamba una maslahi binafsi na hili suala la kurejewa uchaguzi. ungesema mimi ndio katika wale ma cuf wanaopinga uchaguzi kurejewa na ni mmoja wa wanaotaka nchi apewe Maalim.
2. Jamii ya waliowengi hawakuelewi kabisa Salma Said na uzuzu wako. Umesahau wakati wa kupitishwa bajeti ya Serikali. Wapenzi wako wawakilishi wa cuf si walisusia kupitisha bajeti ya SMZ na kutoka nje baada ya kuchukua posho zote za kika cha BLW bila ya maelezo/ sababu ya msingi??? Umelisahau hilo???
3. Nilijua utaelezea pia kwamba Maalim Seif amekuwa akisafiri kila siku kwenda Dar. Pemba South africa kwa pesa ya Serikali na ndege ya serikali na mara nyengine hana hata la maana huko anakokwenda jee mbona hujauliza Maalim anasafiri kwa bajeti ipi na imepitishwa na Baraza gani na wawakilishi gani ikiwa wawakilishi wake wa cuf waligoma na kutopitisha bajeti ya mwaka ja a lengo likiwa ni kuiangusha Serikali ya Dr Shein.
4. Huyu mwanasheria ulie m quote kwenye makala yako Khalid Gwiji mbona hukusema kama alikuwa mgombea wa cuf na ni mwanasheria wa cuf.
5. Bi Salma usipumbaze watu. Kaa kimya Mama. Umesha expire huuziki waka huliki. si wewe wala taarifa zako za kichochezi.
Mwisho.
Wanaume wakishasema uchaguzi upo ujue upo Bi Salma wambie na wenzio kama uchaguzi upo tena mkae mkao wa kula. fedha ipo ya uchaguzi na fedha ipo pia ya kuwashughulikia kuku kama wewe.
Usiharibu nguvu na kalamu yako kujaribu kuharibu masual ya uchaguzi. Babu Jecha ameshavaa suti anasubiri dakika ya kutangaza uchaguzi tuu. kwa taarifa tuu oesa ya uchaguzi imepatikana kutoka Oman kwa Bwana wenu Qaboos. Amechoka kudanganywa na nyie kila siku mnampelekea Serikali sasa kaona bora yaishe kwa salama na amani na kukubali matokeo.
Karibu Sana Bi Salma. Usikurupuke Mama umelala kwenye nyumba ya vigae utaumia.
Ahsante
Mtandao wa Wanyonge waliowengi Zanzibar
http://www.mwananchi.co.tz
Post a Comment