Shirikisho la vyama vya tiba asili Tanzania limesema kuwa halikubaliani na tamko lililotolewa na wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia,wazee na watoto la kukataza matangazo yao.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam mwenyekiti wa Taifa wa shirikisho la vyama vya tiba asili Tanzania Abdulrahman Lutenga amesema kuwa hali hiyo ni kudhalilisha taaluma yao na hivyo bado hawajapata sababu ya kutosha ya serikali kukataza matangazo yao na hawaelewi sababu zilizotolewa.
Chanzo: EATV
Post a Comment