Home » , » Waziri Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga Afanya ziara Jimboni kwake!

Waziri Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga Afanya ziara Jimboni kwake!

Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, January 14, 2016 | 1:46 AM

KITWANGA APOKELEWA KWA SHANGWE USAGARA, AMALIZA ZIARA YAKE MISUNGWI, WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KUMTEUA KUWA WAZIRI

 Wananchi wa Kata ya Usagara, wilayani Misungwi wakimshangilia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga wakati alipokuwa akizungumza na wananchi hao katika Viwanja vya Gulio mjini Usagara. Wananchi hao walimwambia Waziri Kitwanga wanaikumbuka ahadi ya Rais John Magufuli wakati akiwa anamnadi Mbunge huyo kipindi cha kampeni, kuwa suala la maji atalishughulikia Rais mwenyewe. Hivyo wanamuomba Mbunge wao ashirikiane na Rais huyo ili maji yaweze kupatikana kwa haraka zaidi. 

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na wananchi wa Kata ya Usagara kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ya jimbo lake. Kitwanga aliwataka wananchi hao washirikiane katika kuchangia miradi ya maendeleo ili jimbo hilo liweze kupata mafanikio zaidi. Hata hivyo, wananchi hao walimuambia Waziri Kitwanga wanaikumbuka ahadi ya Rais John Magufuli wakati akiwa anamnadi Mbunge huyo kipindi cha kampeni, alisema suala la maji atalishughulikia Rais mwenyewe, hivyo wanamuomba Mbunge wao ashirikiane na Rais huyo ili maji yaweze kupatikana kwa haraka zaidi. Hata hivyo maandalizi ya upatikanaji maji zimeanza jimboni humo.

Msimamizi wa Mradi wa Maji Mwanza, Abbas Muslim akijibu maswali ya wananchi baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga (kulia) kumtaka ajibu maswali ya wananchi hao kuhusu lini maji yatapatikana jimboni humo pamoja na hatua walizozifikia mpaka sasa. 


Chanzo:- Michuzi 

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger