Home » » MKUU WA WILAYA YA KONGWA MH NDEJEMBI AMEANZISHA NAKUZINDUA KAMPENI YA ONDOA NJAA KONGWA (ONJAKO)

MKUU WA WILAYA YA KONGWA MH NDEJEMBI AMEANZISHA NAKUZINDUA KAMPENI YA ONDOA NJAA KONGWA (ONJAKO)

Written By peterdafi.blogspot.com on Sunday, October 30, 2016 | 10:05 AM

MKUU WA WILAYA YA KONGWA MH NDEJEMBI AMEANZISHA NAKUZINDUA KAMPENI YA ONDOA NJAA KONGWA (ONJAKO)

Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi ameanzisha kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO)
Kampeni ambayo itakuwa nikwaajili ya msimu wa Mwaka 2016/2017 na Endelevu kwa Miaka 5.

Mkakati huu unamalengo mahususi ili kukabiliana na Hali ya Ukame.
Kutokana na hayo DC Ndejembi ameagiza kuwa na kilimo cha Mtama zaidi kuliko Mahindi. Kwani Wilaya ya Kongwa ina Kaya 59141, na kila kaya kama ikilima Heka mbili (2) za Mtama, Mavuno itakuwa Tani 71000, za Mtama sawa na 83% ya hitaji la chakula Wilayani Kongwa.

Kutokana na hayo kuna uhitaji wa mazao mengine pia kulingana na maeneo husika.

1. Kuongeza uzalishaji wa mtama toka tani 1/ Hekta mwaka 2016 hadi tani3/hekta ifikapo june 2021,

2. Kuongeza Uzalishaji wa Muhogo mbichi toka tani 6/hekta Mwaka 2016 hadi tani 10 hekta  mwaka 2029

3. Kuongeza uzalishaji wa Alizeti toka tani 1.2/ hekta mwaka 2016 hadi tani 1.8/hekta mwaka 2021

4. Kuongeza uzalishaji wa ufuta toka tani 0.5/hekta mwaka 2016 hadi tani 1.2/hekta ifikapo june 2021

5. Kuongeza pato la Mtu/watu toka Tsh 500,000/= Mwaka 2016 hadi Tsh 800,000/= June 2021.

Akizungumza na Madiwani, Watendaji wa Kata zote 22, Maafisa Tarafa zote 3, Waratibu Elimu Kata, Wenyeviti wa Vijiji vyote 87 vya Wilaya ya kongwa na watendaji wao, pamoja na wadau waalikwa na Kilimo.

DC Ndejembi kawaagiza kuwa ufanywe utaratibu wa kuhakikisha kila kaya inalima Heka zisizopungua mbili (2) za Mtama, Mbili za Mahindi, kulingana na eneo husika wakishauriwa na maafisa ugani lakini mtama ni lazima kwa kila kaya hata kama analima mahindi.

2. Kaagiza kuwa vijana wote wasio na kazi wilayani Kongwa wapewe Hekali mbili mbili ili waache kucheza pool table.

Ameagiza kuwa kuanzia Leo  Marufuku kucheza Pool Table mpaka ifikapo Jioni ya Saa 10, na atakaekaidi hilo sheria stahiki zitachukuliwa.

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger