Home » » WAZIRI UMMY MWALIMU AMEKUTANA NA RAIS NA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA AFYA YA UZAZI WA MPANGO

WAZIRI UMMY MWALIMU AMEKUTANA NA RAIS NA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA AFYA YA UZAZI WA MPANGO

Written By peterdafi.blogspot.com on Monday, October 3, 2016 | 2:08 AM

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais na Mkurugenzi Mkuu wa shirika linaloshughulika na masuala ya Afya ya Uzazi na  Uzazi wa mpango kwa Wanawake na Wasichana  la EngenderHealth Bi. Ulla Muller (wa kwanza kushoto) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika hilo Richard Killian( katikati)

Katika mazungumzo hayo  Waziri Ummy amesema hivi sasa asilimia 27 ya wanawake wa Kitanzania ndio wanaotumia njia za uzazi wa mpango ambapo Serikali ilijiwekea malengo mwaka 2012 kwamba ifikapo mwaka 2020 ifikie asilimia 50 ya matumizi ya njia ya uzazi wa mpango


Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy mwalimu akiongea na Rais pamoja na Mwakilishi mkazi wa Shirika la EngenderHealth walipomtembelea ofisini kwakwe. Waziri Ummy amesema hivi sasa asilimia 27 ya wanawake wa Kitanzania ndio wanaotumia njia za uzazi wa mpango ambapo serikali ilijiwekea malengo mwaka 2012 kwamba ifikapo mwaka 2020 ifikie asilimia 50 ya matumizi ya njia ya uzazi wa mpango.

Rais na Mkurugenzi wa EngenderHealth Bi. Ulla Muller (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo wakati alipomtembelea waziri wa afya na kuzungumza mikakati yao katika upande wa afya,rais huyo atatembelea Mkoa wa Manyara
Mwakilishi Mkazi wa shirika la linaloshughulika na masuala ya Afya ya Uzazi na  Uzazi wa mpango kwa Wanawake na Wasichana  la EngenderHealth Richard Killian( katikati) akizungumza na Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,jinsia,Wazee na Watoto mapema leo kwenye ofisi ya waziri huyo,Kushoto ni Rais na Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo bi. Ulla Muller na kulia ni Waziri Ummy Mwalimu.

(Picha na Wizara ya Afya)

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger