DAS MWAKIPOSA AFUNGUA MASHINDANO YA MPIRA WA PETE WA WASICHANA.
Na Peter Dafi (Arusha)
Katibu Tawala wa Arusha mjini Bw David Mwakiposa, amezindua Mchezo wa Mpira wa Pete wa wasichana.
Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya Babtist Jijini Arusha. Mashindano hayo ya Mpira wa Pete "Netball" yanayohusisha timu nane za Arusha.
DAS Mwakiposa akizungumza na Mabinti na Wanawake zaidi ya Mia mbili (200), waliohudhulia mchezo huo. Amewasihi watumie timu hizo kuunda vikundi vya ujasiriamali, ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na Serikali kupitia Halmashauri ya JIJI la Arusha ya asilimia10% kwa Wasichana na Wavulana.
Katika zoezi hilo alitoa Jezi na Mipira, lakini pia aliahidi kuzifanyia kazi changamoto zao walizowasilisha mapema katika Risala yao.
Aidha, jana alikuwa mgeni Rasmi katika mashindano ya Riadha yanayohusisha Mbio za CROSS COUNTRY. Mashindano yanayoshirikisha wakimbiaji wakike na wakiume, ambapo aligawa zawadi ya fedha na viatu kwa washindi wa kwanza hadi wa sita.
Mwakiposa amewasisitiza vijana hao kuwa wazalendo na kupenda michezo, kwani michezo ni ajira na zaidi hutangaza Nchi. Aliwapongeza Vijana ambao wameiwakilisha vyema Nchi hii katika olimpiki mwaka huu hususani kijana aliyekuwa wa tano.
Aliwaeleza kuwa muda wote wakimuhitaji kwa ushirikiano kamwe Ofisi yake haitasita kuwasikiliza ili kutatua Changamoto zao.
www.peterdafi.blogspot.com
Post a Comment