Home » » KWAHERI CHUMA CHA PUA JOHN SAMWELI SITTA

KWAHERI CHUMA CHA PUA JOHN SAMWELI SITTA

Written By peterdafi.blogspot.com on Monday, November 7, 2016 | 12:05 AM

KWAHERI CHUMA CHA PUA JOHN SAMWELI SITTA.

Sikuwai Kuwa Rafiki yako wala Msaidizi wako.
Niliwai kuwa Mpenzi wa Misimamo yako na Mwanafunzi wako usiemjua Mpaka pale siku nilipokutamkia kuwa Baba! Najifunza mengi toka kwako na Ukasema "KARIBU DAFI KWA KUJIFUNZA ZAIDI MAADILI NA UWONGOZI, KWANI NYIE HASWAA NDIO VIONGOZI WA KESHO"

Awali nilipata Taabu sana Kukufahamu kwa Hadhi na Nyadhifa ulokuwa nazo iliniwia ugumu sana kupata wasaa wakukutana nakuzungumza na wewe CHUMA CHA PUA.

Namshukuru Rafiki yangu na Kaka yangu RC @paulmakonda kwa Mara ya Kwanza alinishika Mkono nakunileta Nyumbani kwako Masaki akanitambulisha kwako na nikachota Hekima na Busara zako.

Hakika Sintosahau Kila Tamshi lililotoka katika Kinywa chako, kwani kila neno lilikuwa ni Somo na Darasa Lenye Zaidi ya PHD ambazo husomwa Darasani.

Nilizaliwa Nzega Mkoani Tabora, Nilipokuwa nakuwa nakupenda Sides niliambiwa! Sikonge kuna Kiongozi mwenye Maono makubwa na vitendo vyakizalendo, Nilikuwa nikiwa nikipata Sifa na nakuona Utendaji wako mkubwa ndani ya Serikali na @ccmtanzania .

Hakika Wana Tabora Tumeondokewa na tumepungukiwa na Kiongozi Mahiri na Nguli wa Siasa kwa Mkoa wa Tabora ambae amejitahidi sana kuiweka Tabora katika Historia yakutoa Viongozi Bora kwa Taifa letu.

Nasema Poleni wana Sikonge, Pole wana Tabora, Pole Tanzania Pole Africa na Dunia Nzima, kwani John Samweli Sitta ni Mmoja tu Wakitofauti. na Hakuna Mwenye kuweza kuziba Pengo lake kamwe.

Nitaikumbuka Daima Falsafa yako ya KAZI KWA VIWANGO, wakakuita MZEE WA VIWANGO, Tanzania imeweka Historia yako ktk Vitabu Mpaka Dunia itakwisha, Daraja la Sarenda, Morogoro Road nk... Hizi ni kazi zako mpaka leo ni bora zaidi na zaidi.

Kwa Ubora wako ulipewa Majina yakishujaa mengi sana, CHUMA CHA PUA, MZEE WA VIWANGI nk....

KWA PAMOJA NAUNGANA Mh. RAIS John Pombe Magufuli KUTOA POLE KWA FAMILIA YA MZEE SITTA KWA KUONDOKEWA NA MPENDWA WAO, POLE KWA SPIKA WA BUNGE, POLE KWA MH MBUNGE WA SIKONGE MAMA SITTA, POLE KWA KAKA NA RAFIKI YANGU MH MSTAHIKI MEYA WA KINONDONI MH BEN SITTA, POLENI SANA FAMILIA YA MZEE SITTA KWA MSIBA HUU MZITO.

BWAMA ALITOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

APUMZIKE KWA AMANI....!

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger