Home » » KAMANDA Kenyela kubariki Mashali vs Sebyala SIKU YA KUMBUKUMBU YA BABA WA TAIFA

KAMANDA Kenyela kubariki Mashali vs Sebyala SIKU YA KUMBUKUMBU YA BABA WA TAIFA

Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, October 10, 2012 | 12:20 AM



KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika pambano la kuwania ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati baina ya Thomas Mashali wa Tanzania na Medi Sebyala wa Uganda litakalopiganwa Oktoba 14,Siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa la Tanzania  kwenye ukumbi wa Friends Corner Manzese jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam , Mratibu wa pambano hilo linalosimamiwa na Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO), Regina Gwae, alisema mbali Kamanda Kenyela, kutakuwa na wageni wengine maalum akiwemo Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azan.
Alisema wanashukuru kwa ushirikiano wa viongozi hao katika maandalizi na hatimaye wamethibitisha ushiriki wao katika pambano hilo ambalo linavuta hisia za watu wengi na wapenzi wa ngumi jijini Dar es Salaam.
Alitaja mapambano manne ya utangulizi ya siku hiyo ambapo Abdul Awilo atazichapa na Shedrack Juma, Selemani Shaaban atavaana na Hamisi Mohamed huku Jonas Segu akinyukana na Ibrahim Class wakati Charles Mashali atatwangana na Teacher Aaron.
“Tumeamua kuchukua mabondia kutoka katika klabu zenye mashabiki wengi, tumechukua kwa Mzazi tumechukua klabu ya manzese anakotoka Mashali na Super D Boxing Club,’ alisema Regina.
Regina alisema, bondia Medi Sebyala na Kocha wake wanatarajiwa kuwasili nchini Oktoba 11 na tayari maandalizi ya safari yao yamekamilika, ikiwemo kuwatumia tiketi na wameshazipokea.
Mratibu huyo, aliishukuru kampuni ya Promasidor wasambazaji wa Sossi Poa, Gazeti la Jambo leo, City Sports Lounge na Times Fm kwa kuwa bega kwa bega kuhakikisha pambano hilo linafanikiwa na kuwa, milango bado iko wazi kwa wadau kujitokeza kufanikisha mchezo huo ambao ni chanzo cha ajira kwa vijana.

 Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema. Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo. 

Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana
mbalimbali

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger