Afisaa mmoja
nchini Kenya ameuawa katika kile polisi wanashuku ni shambulizi la
kulipiza kisasi kufuatia kukamatwa kwa kiongozi wa vuguvugu la MRC
(Mombasa Republican Council) mjini Mombasa, Pwani mwa Kenya
Salim Changu ambaye ni naibu chifu wa eneo hilo
alinyongwa nyumbani kwake katika eneo la Kwale mjini Mombasa, kwa mujibu
wa duru za polisi.Oscar Mwamnuadzi. Alikamatwa baada ya ufyatulianaji risasi katika makao yake mjini humo ambapo polisi waliwaua watu wawili.
Hali ya taharuki imekuwa ikitanda huku uchaguzi mkuu ukikaribia mwezi Machi mwaka ujao.
Zaidi ya watu 100 wameuawa katika ghasia za kikabila Kusini Mashariki mwa eneo la Tana River tangu mwezi Agosti. Ghasia hizo zilisemekana kuwa mbaya zaidi kushuhudiwa tangu kutokea kwa ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007.
Msemaji wa polisi, Aggrey Adoli alisema kuwa Bwana Changu, ambaye ni naibu chifu wa eneo la Kombani, huenda aliuawa na wanachama wa MRC waliomuona kama msaliti.
Mapema wiki jana polisi walianzisha msako mkali dhidi ya wanachama wa vuguvugu hilo, kufuatia madai kuwa wanapanga kutatiza mitihani ya kitaifa
Post a Comment