Papa Benedict anatuma
ujumbe wa maafisa wa Vatican akiwemo askofu mkuu wa New York, Timothy
Dolan -mjini Damascus wiki ijayo katika juhudi za kuitaka serikali na
upinzani nchini humo kuheshimu haki za binadamu katika vita vya wenyewe
kwa wenyewe vinavyoendelea.
Taarifa kutoka Vatican zinasema kuwa Papa
anatuma ujumbe wa ngazi za juu nchini humo kuwafariji watu wote wa taifa
hilo wanaokabiliwa na wakati mgumu na wala sio kundi ndogo tu la
wakristu.Mwakilishi wa papa atakutana na viongozi wa serikali na wale wa waasi.
Mwandishi wa BBC mjini Rome amesema sio jambo la kawaida kwa Vatican kuingilia moja kwa moja katika mzozo kama huo.
Tangazo hili ambalo ni la ghafla lilitolewa wakati wa mkutano wa maaskofu wa kikatoliki mjini Vatican na askofu Tarcisio Bertone, ambaye ni naibu wa Papa.
Ujumbe huo unajumuisha waziri wa mambo ya nje wa Italia pamoja na viongozi wa kanisa hilo kutoka Afrika, Amerika ya Kusini na Bara Asia wote waliohudhuria mkutano wa leo.
Viongozi hao watalenga kukutana na pande zote katika mzozo wa Syria, upande wa upinzani na Serikali ya Assad.
Viongozi wa kikristo nchini Syria walimtumia ujumbe Papa na kumwambia kuwa wakristo nchini humo wanajipata katika hali ngumu sana
Post a Comment