Home » » Ujenzi wa nyumba ya Zuma wachunguzwa

Ujenzi wa nyumba ya Zuma wachunguzwa

Written By peterdafi.blogspot.com on Monday, October 8, 2012 | 2:02 AM



Rais Zuma na wakeze
Uchunguzi umeanza nchini Afrika Kusini kuhusu marekibisho yanayofanywa kwenye nyumba ya binafsi ya Rais Jacob Zuma, ujenzi utaogharimiwa na serikali.
Tangazo limetolewa na ofisi ya mhifadhi wa masilahi ya wananchi, baada ya magazeti kutuhumu kwamba ukarabati unaopangwa kufanywa kwenye nyumba ya Rais Zuma utaogharimu dola milioni 25, karibu wote unatarajiwa kulipwa na serikali.
Msemaji alieleza kuwa kamati ya uchunguzi imewasiliana na ofisi ya rais kuhusu ujenzi huo kwenye nyumba ya Rais Zuma ilioko Nkandla katika jimbo la KwaZulu-Natal.
Serikali ya Afrika Kusini inasema ujenzi huo unafuata kanuni rasmi.

Na BBC
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger