Uchunguzi umeanza nchini Afrika
Kusini kuhusu marekibisho yanayofanywa kwenye nyumba ya binafsi ya Rais
Jacob Zuma, ujenzi utaogharimiwa na serikali.
Tangazo limetolewa na ofisi ya mhifadhi wa
masilahi ya wananchi, baada ya magazeti kutuhumu kwamba ukarabati
unaopangwa kufanywa kwenye nyumba ya Rais Zuma utaogharimu dola milioni
25, karibu wote unatarajiwa kulipwa na serikali.Msemaji alieleza kuwa kamati ya uchunguzi imewasiliana na ofisi ya rais kuhusu ujenzi huo kwenye nyumba ya Rais Zuma ilioko Nkandla katika jimbo la KwaZulu-Natal.
Serikali ya Afrika Kusini inasema ujenzi huo unafuata kanuni rasmi.
Na BBC
Post a Comment