Home » » Wachimba migodi 8,000 wafutwa kazi A.Kusini

Wachimba migodi 8,000 wafutwa kazi A.Kusini

Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, October 24, 2012 | 6:33 AM

Mamia ya wachimba migodi wamekataa kurejea kazini na hivyo kufutwa kazi
Zaidi ya wachimba migodi 8,000 waliokuwa wanagoma , nchini Afrika Kusini, wamefutwa kazi baada ya kukataa kurejea kazini.
Wamiliki wa mgodi wa Gold Fields wamesema kuwa wafanyakazi hao walipuuza makataa ya jana saa kumi jioni kurejea kazini ndipo wakafutwa kazi
Sekta ya mdini nchini Afrika Kusini ilikumwba na migomo pamoja na vurugu na kusababisha vifo vya watu hamisni.
Wafanyakazi wamekuwa wakidai nyongeza ya mishahara na mazingira bora ya kazi ingawa hatua iliyochukuliwa kuhusu mgodi wa KDC East, Magharibi mwa Johannesburg -inahusiana na vyama vya wafanyakazi wala sio mishahara.
"wafanyakazi wote 8,500 waliokuwa wamegoma, hawakurejea kazini '' alisema msemaji wa kampuni hiyo, Sven Lunsche.
"Hawakurejea kazini kwa hivyo tumewapa wote barua za kuwaachisha kazi.'' Aliongeza kuwa wafanyakazi hao wana siku moja kukata rufaa
"sasa tumefika sehemu ambapo hatuwezi kuwa wavumilivu tena . Tumelazimika kuchukua hatua na tumefanya hivyo, " alisema bwana Lunsche.
"tunachunguza hali na tuna polisi walio tayari kuchukua hatua ikiwa vurugu litatokea. Lakini kufikia sasa mambo yako shwari.''
Kampuni ya Gold Fields ilitoa onyo la mwisho kwa wafanyakazi kwenda kazini kuanzia Jumatatu tarehe 22 mwezi huu au wachukuliwe hatua.
Kampuni hiyo ilipata kibali kutoka kwa mahakama kutaja mgomo wao haramu.
Migomo katika sekta ya madini nchini Afrika Kusini imeathiri sana uchumi wa nchi hiyo huku sarafu ya nchi ikipoteza thamani.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger