Mhe Mizengo Pinda leo bungeni kwenye kipindi cha maswali na majibu
ameeleza waziwazi kuwa kuna haja ya kuwakabili viongozi wa kisiasa.
Katika kulidadavua hilo ametolea mfano kauli ya Dr Slaa aliyoitoa baada
ya kushindwa kwenye uchaguzi mkuu, kauli hiyo ni ile iliyosema "nchi
haita tawalika".
Lakini pia ameongezea ya kuwa,"kama wananchi watakaidi kauli ya vyombo
vya dola ya kuwataka waache vurugu, basi naagiza vyombo vya dola
viwapige tu, kwani hatuwezi kuendelea hivi."
Akijibu swali la mh mangungu,mb. Waziri mkuu mizengo pinda amesema
matukio ya kigaidi na uvunjifu wa amani yanayoendelea hapa nchini hivi
sasa ni mwendelezo na utekelezaji wa kauli ya nchi haitatawalika
iliyotolewa na chadema baada ya kushindwa uchaguzi mkuu 2010 na wakati
wanaingia bungeni walitoa kauli hiyo..pinda amesema serikali imevumilia
vya kutosha sasa basi..dola iachwe ichukue hatua za kurudisha amani ya
nchi kwani vita ikitokea hakuna atakayebaki salama, tutaathirika wote.
Amesema atakayevunja sheria na kusababishwa vurugu lazima akutane na
virungu vya polisi.
Lakini pia ameongezea ya kuwa,"kama wananchi watakaidi kauli ya vyombo
vya dola ya kuwataka waache vurugu, basi naagiza vyombo vya dola
viwapige tu, kwani hatuwezi kuendelea hivi."
My take. Sasa serikali ipo kazini kulinda na
kudumisha amani. Tuipe ushirikiano
Post a Comment