Sasa tembo wameamua kujilinda. Juzi, tembo mmoja amewaua majangili
wawili waliotaka kumuua. Tukio hilo limetokea katika Hifadhi ya Taifa ya
Mikumi-upande wa Kilosa. Mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa Mjangili
hayo yalipita kijijini kwao yakielekea hifadhini kwa ajili ya kuua tembo
yakiwa na silaha nzito.
Inadaiwa kuwa tembo aliyewaua majangili alijeruhiwa kwa risasi na
kujifanya amekufa.Majangili waliposogea kwa ajili ya kutimiza lengo lao
la kuchukua nyara,tembo husika alikurupuka na kuanza kuwashambulia
majangili hao hadi kuwaua wote wawili.Halafu, akaziponda maiti na
kurundika miti katika maiti hizokiasi cha kuzifanya zisionekane.
Mashuhuda waliofika katika eneo la tukio walikuta maiti hizo pamoja na
silaha walizokuwa nazo majangili hao. Natoa pongezi kwa tembo wa Mikumi
kwa kujilinda. Tembo wote nchini nao waige mfano huo.
Chanzo: Wananchi wanaoishi kandokando ya Mikumi,upande wa Kilosa na Askari Wanyamapori
TEMBO auwa Majangili....!!
Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, January 28, 2014 | 2:11 AM
Related Articles
- WARAKA No. 2 WA MHE. SPIKA KUHUSU UGONJWA WA CORONA
- UVCCM CHAMWINO WAJAZA FOMU KWA NIABA YA BARAZA LA WADHAMINI
- MAVUNDE APOKEA MIFUKO 724 YA SARUJI KUTOKA CRDB BANK
- TANZIA: Mwanajeshi wa Tanzania auawa na wengine watano hali ni mbaya
- Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe Christine Mndeme , leo tarehe 3/6/2018 amekabidhiwa Mwenge wa Uhuru Na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe Christopher Ole Sendeka.
- AJALI MBAYA YAUWA MAAFISA WA SERIKALI
Labels:
kitaifa
Post a Comment