Home » , » Paul Makonda Alia na Ongezeko la Posho za wabunge wakatiba.

Paul Makonda Alia na Ongezeko la Posho za wabunge wakatiba.

Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, February 20, 2014 | 8:31 AM

Paul Makonda ni Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM Taifa.
Ni kijana Makini sana na Hodari kwa kila afanyacho huitaji kufanya kwa Kiwango cha juu, Pia ni Kijana mwenye Misimamo yake Imara na Thabiti si Mtu wakuyumbishwa yumbishwa na kununuliwa kama vijana wengi wanunuliwavyo.
Kwani amekuwa akitamka na kufanya mambo mengi sana kwa ajili ya jamii na Chama pia, hii humfanya azidi kuwa mwanasiasa Mkomavu sana.

Leo hii http://peterdafi.blogspot.com/ imezungumza nae kuhusu Posho za Wabunge wakatiba, Tuimemtafuta kwakuwa Yeye ni Mmoja kati ya wabunge wa Bunge hili na Katiba  na yuko Dodoma Tangu Tarehe 14 mwezi huu wa Pili hii nikuonyesha uhodari wa Jambo alilonalo mbele yake.

KUHUSU POSHO

Makonda anasema Laki tatu ni pesa ndogo kwa Posho za Wabunge hawa wanapokuwa Dodoma, kwani matumizi ni mengi sana kulinganisha namatumizi yao wanapokuwa Dodoma, Kwani.....

1 Laki tatu(300,000) haitoshi, na mimi nasimamia hilo hadi iongezwe hii kazi ni ngumu. watu wamekuja na wanasheria wasaidizi ili kuwasaidia na kuwashauri.
2. Malipo ya dereva na Posho pia chakula
3. Nyumba za wageni Dodoma na Hotel zote zimejaa na vyumba vimepanda bei si chini ya elfu (40,000Tsh). na kuendelea....
4. Mafuta ya Gari...
5. Mtu umeacha kazi zako na familia unakaa Dodoma kwa miezi miwili(2).
6. Unasomesha watoto Ada za Shule na Matumizi ya Familia na watoto, Hapo haijaja Dharula ya watoto Kuumwa nk...

Kwa hali hii Serikali lazima ilitizame swala hili vizuri apo ndo Watu watakaa vizuri Bungeni Dodoma na kufanya kazi hii vema kwa Moyo Mmoja wa Dhati.


Alisema Makonda Jioni hii ya Leo nilipozungumza nae kwa Simu.

Leo hii magazeti mengi sana yamechapisha habari za Posho kuwa ni Nyingi nk...

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger