Home » , » Taifa Jogging na Sports Club Tanzania Nzima waungana na Kupokelewa na Dk Hamisi Kigwangalla Mnazi Mmoja Leo.

Taifa Jogging na Sports Club Tanzania Nzima waungana na Kupokelewa na Dk Hamisi Kigwangalla Mnazi Mmoja Leo.

Written By peterdafi.blogspot.com on Sunday, November 2, 2014 | 1:33 AM

Mgeni Rasmi Dk Hamisi Kigwangalla Asisitizia Amani Na Upendo Kwa Taifa Letu.

Awaomba Wanasiasa Wenzie Kuheshimu Taifa Letu Na Kuacha Amani Na Upendo Iendelee Kutawala Nchini.

Amesema kuwa Wanasiasa wanaweza Kuivuruga Amani ya Nchi hii kama Hawatakatumia Hekima Na Busara ktk Hotuba Na Vitendo Vyao kwani Wananchi huwasikiliza Na Kuwafuata Wanaowaongoza (Viongozi wao) hivo Kaomba tudumishe Amani Na Upendo.
Pili Kigwangalla Kauomba Uongozi wa Taifa Jogging Kuunda Mashirikisho ya Jogging Tanzania Bara Na Visiwani Na Atasaidia Mchango wa Kusajili Mashirikisho Mayo Kwa Kuwapa Million I Moja Moja Kwa Ajili ya Usajili Na Millioni Tatu Tanzania Bara Na Million I Mbili Tanzania Visiwani Ili Wafungue SACCOs zao Kwa Ajili ya Kukopeshana.
Lengo ni Kama Kuna Tatizo Kwa Mwanakikundi au Kuna Sherehe Basi Waweze Saidiana Kwa Kupitia Mfuko wa Kundi LA Jogging.

Tatu Mh Kigwangalla Amesema Kafurahishwa sana Na Ummoja wao wa Kufanya Mazoezi Na Kuimarisha Afya zao Kwani inawafanya wawe Viongozi Na Viajana hata Wazee Imara Na Thabiti sana.
Ivo Kasisitiza sana Kufanya mazoezi Kwa Watanzania Wote.

Kwa Upande wake Mzee Malinzi Mwenyekiti Msaafu wa Taifa Jogging & Sports Club amesema Anampongeza sana Mh Kigwangalla Kwa Kuwa Ni Kijana Mbunge mwenye Kujitambua Na Kujitoa Zaidi.
Mzee Malinzi Amemuomba Mh Kigwangalla Mbunge wa Nzega Na Mwenyekiti TAMISEMI kuwa Asimsahau ktk Ufalme wake.

Kwa Upande wake Mzee Kipingu kasema Anamfahamu sana Kigwangalla ni Kiongozi Mwenye Misimamo Sana Na Mwenye Kusimamia Ukweli ivo Atafika Mbali.

Tamasha hili Hufanyika Kila Mwaka Na Kwabahati Nzuri sasaivi Chama hiki kimefanikiwa Kusajiliwa Na Kutambulika Kiserikali.

Kigwangalla Pia Kachangia Damu Salama Leo

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger