Ajali mbaya yatokea maeneo ya Mafinga Iringa
sehemu kunaitwa Changarawe ambapo gari
aina lori lilokuwa likitokea Dar kwenda Mbeya
ambapo lilikuwa likikwepa shimo kubwa lililopo
katikati ya barabara na kugongana na gari la
abiria la Kampuni ya Majinja lililokuwa likitoka
Mbeya kwenda Dar. Hii ni maelezo ya trafki
aliyepo hapa.
Kontena la lori limelalia kabisa basi, na watu
wengine wamelaliwa na wengine
wameporomokea korongoni, mpaka sasa
hakuna majeruhi ni maiti tu, wala hakuna mtu
ambaye inadhaniwa amepona.
- Kuna watoto wawili hapa, makadirio ya miaka
ni mitatu na saba, lakini hawa inasemekana
kwamba walirushwa korongoni kutokana na huo
mgongano.
- Uokoaji wa maiti na majeruhi walionasa
kwenye ajali hapa eneo la tukio unazorota
kutokana na ukosefu wa Gesi ya kukata basi
kukosekana Mafinga. Juhudi zinafanyika ili
kuweza kuokoa majeruhi pamoja na maiti.
Ajali mbaya ya Basi na Roli imetokea Mafinga Iringa
Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, March 11, 2015 | 3:57 AM
Related Articles
- Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe Christine Mndeme , leo tarehe 3/6/2018 amekabidhiwa Mwenge wa Uhuru Na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe Christopher Ole Sendeka.
- AJALI MBAYA YAUWA MAAFISA WA SERIKALI
- KIFO CHA AKWILINA NI MTAJI WA SIASA KWA WANASIASA UCHWALA WA TANZANIA.
- SIKU YA USAFI,UVCCM WAMEFANYA USAFI OFISI YA DC CHAMWINO.
- WARAKA No. 2 WA MHE. SPIKA KUHUSU UGONJWA WA CORONA
- UVCCM CHAMWINO WAJAZA FOMU KWA NIABA YA BARAZA LA WADHAMINI
Labels:
kitaifa
Post a Comment