Ghafla
isivyo tarajiwa, bilionea mmoja nchini Hong Kong amejitolea kumwaga
dola milioni kwa 64 sawa na Paundi milioni 40 ambapo kwa hela zetu za
madafu ni bilioni 120, na milioni 400 kwa mwanaume yeyote
atakayejitokeza kumuoa binti yake mwenye tabia za kisagaji.
Tajiri
huyo mfanyabiashara yuko tayari kutoa mkwanja huo wa hatari kwa mtu
atakayemchukua binti huyo ila awe mwerevu, msomi na asiwe ni kwa nia za
kujitafutia kipato.
Papaa
huyo wa China Cecil Chao Sze-tsung amefikia hatua hiyo kufuatia taarifa
kumfikia kuwa binti yake huyo Chao ana mahusiano ya kimapenzi na Sean
Yeung uliodumu kwa muda wa miaka saba (7) nchini Ufaransa.
Binti
huyo Chao ambaye ni Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Manchester na pia
Mkurugenzi wa Makampuni na Biashara za Baba yake, Anaendesha Kampuni ya
walimbwende ya Monde Talent na pia Afisa Uhusiano wa kampuni kubwa
nchini Hong Kong.
Hata hivyo Bilionea Cecil Chao amesema hamlazimishi binti yake kuolewa ila atakayejitokeza atakula bingo.
Sean Yeung akiwa na mpenzi wake.
Baba na Mwana.
Post a Comment