Chelsea imekuwa timu ya kwanza
kuichapa Arsenal katika mechi za ligi kuu ya Uingereza msimu huu baada
ya kuwachapa 1-2 katika uwanja wao wa nyumbani,Emirates siku ya
Jumamosi.
Vijana wa Roberto Di Matteo ndio walikuwa wa
kwanza kufunga katika dakika ya 20 kupitia mshambulizi Fernando Torres
baada ya mkwaju wa adhabu kupigwa na Juan Mata.Na katika dakika ya 52 ya kipindi cha pili, Mata alipiga mkwaju mwengine wa adhabu ambapo ulimshinda mlinzi Laurent Koscielny na badala yake kumgonga mguu na kuingia ndani huku ikimuacha Kiper wa Arsenal Vito Mannone hoi.
Wenger amekua akilalamika kwamba safu yake ya nyuma imekuwa ikizembea katika mipira ya adhabu.
Licha ya kufungwa huko, Arsenal walitawala ngoma hiyo nzima ya Jumamosi lakini safu ya mbele ya vijana hao wa Arsene Wenger iliyonekana kukosa makali na kuwa na kukosa umakini.
Post a Comment