Home » , » MATOKEO YA CCM NZEGA NA WAJUMBE WA NEC HAYA HAPA...!!

MATOKEO YA CCM NZEGA NA WAJUMBE WA NEC HAYA HAPA...!!

Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, October 2, 2012 | 9:37 PM


Aliyeshinda ni Ndg. Amos Majile Kanuda (Mwenyekiti wa CCM Wilaya) na Ndg. Yasin Said Membar (MNEC) yani Mjumbe wa NEC, na pia Ndg. Richard Mayunga (amechaguliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya, Siasa, Itikadi na Uenezi, na Ndg. Majaliwa Bilal Ismail amechaguliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Nzega, Uchumi na Fedha
 Kwa hali hiyo matokeo yalikuwa hivi...!!

Kanuda alipata kura 1486, Francisko Kulwa Shija kura 588, Patrick Joseph Bulabuza kura 38 , kwa nafasi ya Uenyekiti na MNEC sikumbuki kura zao ila waligombea watu watatu Emmanuel Misigalo, Yassin Said Membar na Paul Kabelele, uchaguzi wa kwanza aliongoza Misigalo akafuatiwa na Membar lakini hakuvuka nusu hivyo ngoma ikarudiwa, na hapo ndipo Membar aliposhinda kwa kura zaidi ya 1000 na mwenzake Misigalo alipobaki na ushindi wa kura 400 na ushee
 Na hivi ndivo alivyoandika katika ukurasa wake wa FB Mbunge wa Nzega baada ya matokeo hayo...!!!
Hamisi Kigwangalla 
Mara baada ya fununu za matokeo ya uchaguzi kuwa wazi kuna watu wawili maarufu walizimia, na walipozinduka waliangua vilio na hawajaonekana Nzega tena...tunawapa pole na kuwatakia quick recovery huko waliko! Huo ndiyo ushindani...na sisi tunawaambia kuwa wasihofu kitu watatendewa haki siku zote katika chama hiki na katika uongozi huu. Malengo yetu ilikuwa ni kuondoa watu wa hovyo, wachumia tumbo n
a wanaofanya kazi kwa maelekezo ya mtu mmoja tu na sasa kuweka watu makini na mahiri watakaokisimamisha chama, hata kama itamaanisha kuniadhibu mimi pale itakapobidi...Chama Kwanza, Mtu baadaye! Hakuna mtu maarufu na wa maana ndani ya CCM kuliko CCM yenyewe. Nimesikia wanataka kuikimbia nchi, tunawasihi wasifanye hivyo, waendelee tu kuwa waadilifu na waaminifu kwa chama na kwa nchi na ipo siku mambo yao yatawanyookea tu!


Muheshimiwa mbunge amekuwa akisimama kidete tangu uchaguzi umeanza mpaka matokeo hayo kutoka ninguvu yake ya na ukomavu wake wa Siasa umetoa majibu haya.


 
Mh, Hamisi Kigwangalla
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger