Home » » Utulivu Eritrea baada ya wanajeshi kuasi

Utulivu Eritrea baada ya wanajeshi kuasi

Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, January 22, 2013 | 6:46 AM



Wakuu nchini Eritrea wanasema mji mkuu Asmara umesalia tulivu, siku moja baada ya wanajeshi mia mbili walioaasi kuteka wizara ya habari.
Afisa mmoja mkuu Yemane Gebremeskela aliliambia Shirika la habari la Ufaransa kuwa hali ni shwari kama ilivyokuwa awali.
Runinga ya kitaifa imerejea hewani baada ya matangazo kukatizwa na taarifa kutolewa ya kutaka kuwachiliwa huru kwa wafungwa wote wa kisiasa na kutekelezwa kwa katiba.
Bwana Yemane Gebremeskel, aliliambia shirika la habari la Ufaransa kwamba hali ni shwari katika Jiji la Asmara tangu siku ya Jumatatu.
Lakini afisa mwingine alisema kumekuwa na matukio machache.
Hata hivyo hali ni tofauti tangu wanajeshi 200 walioasi walipovamia wizara ya habari kutatiza matangazo ya radio na televisheni na kuwalazimisha watangazaji kusoma taarifa inayohimiza kuachiliwa huru kwa wafungwa wa kisiasa.
Matangazo ya Televisheni ya taifa sasa yamerudi hewani na mabalozi wa mataifa ya magharibi nao wamethibitisha kuwa waasi hao tayari wameondoka kutoka kwenye jumba la wizara hiyo ya habari.
Hata hivyo, kufikia sasa bado haijajulikana hatua waliZochukuliwa wanajeshi hao waasi.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger