Home » »

Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, January 22, 2013 | 6:58 AM



Wilfred Saha
Manchester United inatarajiwa kuendeza mazungumzo na klabu ya Cystal Palce, kuhusu usajili wa mchezaji kiungo wake Wilfred Saha.
Sir Alex Ferguson, amasalia nchini England huku Manchester United ikisafiri kwenda nchini Qatar kwa mazoezi zaidi.
Ripoti zinasema Manchester United, ipo tayari kulipa pauni milioni kumi na mbili, kumsajili mchezaji huyo na wakati huo huo, imruhusu kuendelea kuicheza Cystal Palace hadi mwisho wa msimu huu.
Hata hivyo, vilabu hivyo viwili havijatoa taarifa yoyote kuhusu mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20.
Duru zinasema vilbau hivyo huenda vikaafikiana kufikia mwisho wa wiki hii kuhusu usajili wa mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uingereza.
Zaha, ambaye amekuwa akipata mafunzo katika chuo cha Cystal Palace cha Selhurst Park, amefunga magoli 15 baada ya kuichezea mechi 124 na alicheza mechi yake ya kwanza mwaka wa 2010.
Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson
Saha alitajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka mwaka wa 2012 kwa wachezaji wanaoshiriki katika ligi daraja ya kwanza na vilabu kadhaa vinavyoshiriki katika ligi kuu ya Premier vimeripotiwa kutaka kumsajili mchezaji huyo.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger, amesema amekuwa akimchunguza mchezaji huyo lakini amesisitiza kuwa klabu hiyo halijawasilisha ombi lolote la kutaka kumsajili.
Crystal Palace inashikilia nafasi ya nne kwenye ligi daraja ya kwanza, alama mbili tu, chini ya alama zinazohitajika ili kupandishwa daraja msimu ujao, na endapo Saha atakihama klabu hiyo sasa itakuwa pigo kubwa katika harakati zao ya kuwania nafasi katika ligi kuu ya premier msimu ujao.
Zaha amekuwa na klabu hiyo tangu alipokuwa na umri wa miaka 12 na ni miongoni mwa wachezaji waliokuzwa na klabu hiyo na kwa sasa anafuata mkondo wa mcheza kiungo wa Chelsea Victor Moses na Nathaniel Clyne wa Southampton.
Aliyekuwa mshambulizi wa timu hiyo Mark Bright, amemtaja Saha kama mchezaji bora zaidi kuwahi kukuzwa na klabu hiyo tangu enzi za mshambulizi wa Uingereza Ian Wright.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger