Test Footer

Habari Mpya

CCM na CHADEMA kimewaka tena mkoani SHINYANGA wilaya ya KAHAMA

Written By peterdafi.blogspot.com on Thursday, February 28, 2013 | 2:35 AM


Chama cha demekrasia na maendeleo CHADEMA Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kinataraji kufanya maandamano ya amani marchi 02 mwaka huu, kuukumbusha uongozi wa mgodi wa Buzwagi kuwaunganishia umeme wananchi wa Kahama, kutoka katika mgodi huo.

Maandamano hayo pia yanalengo la kuukumbusha uongozi wa Mgodi kuishinikiza serikali kusiamamia utekelezaji wa ujenzi wa barabara za mji wa Kahama kwa kiwango cha lami.

Kufuatia chadema kutaka kufanya maandamano hayo chama cha mapinduzi kimesema chadema wanataka kufanya hivyo baada ya kupata taarifa kuwa tayari serikali ya ccm imeshakamilisha zoezi hilo na utekelezaji utaanza wakati wowote hivyo chadema wanataka kufanya maandamano ili umeme huo ukifikishwa kahama na barabara zikianza kujengwa waseme ni mafanikio ya maandamano yao.

lakini pia ccm wamesema chadema huenda wanataka kufanya maandamano ili kumuudhi muwekezaji huyo na kuchelewesha utekelezaji huo.

Barcelona yakaangwa na Real Madrid

Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, February 27, 2013 | 6:24 AM



  
Wachezaji wa Real Madrid wakisherehekea bao lao
Real Madrid imedhihirisha kuwa bado ingali mbabe wa soka nchini Uhispania baada ya kuilaza Barcelona kwa magoli matatu kwa moja katika mechi kali ya marudiano ya kuwania kombe la Copa del Rey siku ya Jumanne usiku katika uwanja wa Nou Camp.
Cristiano Ronaldo aliifungia Real Madrid bao lao la kwanza kupitia mkwaju wa penalti baada ya kuangushwa kwenye eneo la hatari na mlinda lango wa Barcelona Gerard Pique.
Juhudi za nyota wa Barcelona Lionel Messi kusawazisha ziliambulia patupu pale mikwaju yake ikidakwa na kipa wa Real Madrid.
Ronaldo aliizidhishia Barca masaibu pale alipofunga bao la pili baada ya kupata pasi kutoka kwa Angel di Maria.
Matatizo ya Barcelona hayakuishia hapo na mshambulizi wa real Raphael Varane alifunga bao la tatu kwa kichwa na hivyo kuhakikisha kuwa Real inasonga mbele ya mashindano hayo.
Kufikia sasa Real imo alama 16 nyuma ya Barcelona katika msururu wa ligi kuu ya la liga na wiki ijayo imepangiwa kuchuana na Manchester United katika mechi ya marudiano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani ulaya.
Real sasa imejikatia tikiti ya fainali ya mashindano hayo ya Copa del Rey na itacheza dhidi yuan mshindi wa mechi kati ya Sevilla na Atletico Madrid.
Kati ya mechi kumi kati ta timu hizo mbili, Barcelona ilikuwa imeshunda mechi tano na katika mechi ya hiyo, Real Madrid ilitawaka kwa kiasi kikubwa.

Watu 35 wafariki katika ajali ya basi Kenya



Basi hilo lilikuwa linaelekea Mandera na Garissa
Takriban watu 35 wameuawa katika ajali ya barabarani karibu na mji wa Mwingi Mashariki mwa Kenya.
Duru za polisi zilisema kuwa wengi wa waliofariki walikuwa wanafanya kazi mjini Nairobi, na walikuwa wanarejea makwao kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika siku ya Jumatatu.
Farah Aden Ali, aliyenusurika kifo alisema kuwa basi hilo lilikuwa limejaa watu kupindukia na lilianguka baada ya dereva kupoteza mwelekeo.
Barabara nyingi nchini Kenya ziko katika hali mbaya na vile vile hali ya mabasi mengi ni mbaya.
Afisaa wa trafiki Samuel Kimaru alisema kuwa takriban abiria 35 walifariki na wengine 50 kujeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo.
Bwana Aden Ali aliambia BBC kuwa vikundi vya uokozi viliwasili katika eneo la ajali masaa manne baada ya ajali kutokea hali iliyosababisha waliokuwa wamekwama ndani ya basi hilo kufariki.
Basi lilikuwa limejaa watu na lilikuwa linaelekea katika miji ya Mandera na Garisa
Ali alisema kuwa dereva alikuwa na matatatizo na gia ya basi hilo tangu kundoka Nairobi
Alisema alikuwa amelala lakini aliamka muda mfupi baada ya ajali kutokea.
''Dereva alipoteza mwelekeo. Alikua anajaribu kulirejesha basi barabarani , lakini likaanguka kwa upande,'' alisema Ali.
Babaraba za Kenya huwa na msongamano mkubwa wa magari hususan kabla ya uchaguzi mkuu huku wafanyakazi wa miji wakielekea mashinani kupiga kura.

Slaa apinga madiwani CHADEMA kufukuzwa

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Makao Makuu kimepinga maamuzi ya Kamati ya Utendaji ya Chama hicho Wilaya ya Musoma cha kuwavua Uanachama madiwani wawili wa viti maalum Habiba Ally Zeddy na Mariam Daudi Chacha na hivyo kupoteza sifa ya kuwa madiwani kwa mujibu wa Katiba ya Chama hicho. Katika barua iliyotumwa na Afisa Sheria wa Chama hicho Ester Daffi yenye kumbukumbu namba C/HQ/M/MARA/10/101 ya tarehe 22/2/2013 kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Chama hicho Willbord Slaa ilisema kama kuna utovu wa nidhamu kwa wahusika ilitakiwa kuzingatia masharti ya Katiba na Kanuni hasa kanuni ya Uendeshaji kazi za Chama ibara ya 6.5.2 pamoja na Kanuni ya 8.0 (a) na (b) ya nidhamu kwa madiwani. Katika barua hiyo ilidai suala hilo lilitakiwa kutolewa taarifa Makao Makuu kwa ajili ya kuwasilishwa kwenye Kamati Kuu kwa ajili ya maamuzi kwa kuwa mamlaka ya kuwavua Uanachama yanapaswa kuzingatia kanuni tajwa ya katiba ya Chama hicho. Alisema Makao Makuu ya Chama hicho imepinga maamuzi hayo kutokana na madiwani hao kukata rufaa kupinga maamuzi hayo katika barua yao ya rufaa iliyotumwa kwa njia ya nukushi tarehe 21/2/2013 na kuipitia kwa kina na kisha kutoa maamuzi hayo kwa mujibu wa katiba. Ilidaiwa katika barua hiyo ambayo nakala yake imepelekwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma ilisema kamati ya Utendaji ya Chadema Wilaya ya Musoma haikuzingatia barua kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama hicho ya tarehe 16/2/2013 yenye kumbukumbu namba C/HQ/M/MARA/101. Katika barua hiyo iliyokuwa na kichwa cha Habari (MGOGORO NDANI YA HALIMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA) ilidai tarehe 15/2/2013 Mkao Makuu ilipokea taarifa kutoka kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Musoma Alex Kisurura kuhusu mgogoro unaoendelea ndani ya ya Halimashauri hiyo ukihusisha baadhi ya Viongozi wa Chama wa Jimbo. Katika barua hiyo ilidai Halimashauri ya Manispaa ya Musoma inaongozwa na (CHADEMA) na kwa mujibu wa kanuni ibara ya 3.1 (a) (c) (g) na (i) ya kanuni za kusimamia Shughuli,Mwenendo na Maadili ya Halimashauri zilizo chini ya Chadema,Ofisi ya Katibu Mkuu kwa azimio la Kamati Kuu ndiyo msimamizi wa shughuli za Halimashauri za Chadema Nchini. Barua hiyo ilida Agenda kuhusu mgogoro ndani ya Halimashauri au kutofautiana kwa Meya na madiwani na au Uongozi wa Chama isijadiliwe mpaka mchakato wa ndani ya Chama utakapokamilika au kwa maelezo kutoka Makao Makuu na pindi itakapokwenda kinyume hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama zitachukuliwa dhidi ya wote watakaokiuka maelezo yaliyotolewa. Akizungumza na blog hii mara baada ya kupokea barua ya majibu ya rufaa kutoka Mkao Makuu ya Chadema,Diwani Habiba Ally Zeddy alisema licha kushinda rufaa yao ya kuvuliwa Uanachama Makao Makuu inapaswa kuangalia kwa karibu mwenendo wa Chama hicho Wilaya ya Musoma. Alisema maamuzi ya kuvuliwa Uanachama waliyofanya Kamati ya Utendaji na kutangazwa katika Vyombo vya Habari ni kama wamezalilishwa kwani hadi sasa licha kutolewa maamuzi ya kuvuliwa hakuna barua yoyote waliyopewa kuhusu kuvuliwa Uanachama na kukosa sifa ya kuwa madiwani. Chanzo Jamii Forum

Tamko la Jumuiya za Kiislam kuhusu mauaji ya Viongozi wa Dini na uchochezi wa Vyombo vya Habari

 
TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU ZANZIBAR KULAANI MASHAMBULIZI NAMAUAJI YA VIONGOZI WA DINI PAMOJA NA KUPINGA KAULI ZA UCHOCHEZI DHIDI YAZANZIBAR

Kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu Mlezi wa Viumbe. Sala na salamu zimfikie Mtume wetu Mtukufu Muhammad (S.A.W), jamaa zake, maswahaba zake waongofu na wote wanaowafuata kwa wema hadi Siku ya Malipo.

Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar lililokaa Jumapili tarehe23/2/2013 katika kikao cha kutathmini matukio ya kushambuliwa na kuuliwa viongozi wa Dini yakiwemo ya karibuni ya kupigwa risasi na kuuliwa Padri Mushi pamoja na kupigwa mapanga na kuuliwa Sheikh Ali Khamis Bin Ali Khatibu wa Mwakaje na kuendelea kutolewa kwa kauli za uchochezi dhidi ya Zanzibar linatamka ifuatavyo:

1. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linalaani vikali na kwa nguvu zote matukio ya kushambuliwa na kuuliwa viongozi wa Dini likiwemo tukio la karibuni la kupigwa risasi na kuuwawa Padri Mushi kulikofanywa na wahalifu wasioitakia mema Zanzibar.


2. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linapenda kuweka wazi kuwa uhai ni tunu kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu aliyotunukiwa binaadamu hivyo hakuna mwenye mamlaka ya kuiondoa haki hiyo isipokuwa yeye mweyewe Mwenyezi Mungu. Kutokana na ukweli huu ndio maana Sheria za Kiislamu zimeweka wazi mtu mwenye kumuuwa mwenziwe naye auliwe kama inavyoelezwa katika Kitabu kitufu cha Quran kama ifuatavyo:

“Na humo (katika Taurati) tuliwaandikia ya kwamba mtu (huuwawa kwa sababu yakuuwa mtu) kwa mtu, ……….” (5:44)

Hivyo, vitendo vya kiharamia vya kushambuliwa viongozi wa Dini kulikoanziakwa kumwagiwa tindikali Sheikh Soraga, kupigwa risasi Padri Ambrose Mkenda, kuuliwa Padri huko Musoma, kupigwa risasi na kuuwawa Padri Mushi na kushambuliwa kwa mapanga na kuuliwa Sheikh Ali Khamis Bin Ali Khatibu wa Mwakaje kwa dhulma kulikofanywa na wahalifu ni jambo lisilokubalika na Uislamu na Waislamu wenyewe. Aidha wahusika wa matendo haya wawe wafuasi wa Dini yoyoteile bado watahesabika ni wahalifu kwani vitendo vya kihalifu na kiharamia kamwehaviwezi kunasibishwa na Dini fulani.

3. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linaviomba vyombohusika kufanya upelelezi wa kina kuhusu matukio haya kwa kuzingatia uadilifu namisingi ya kazi zao ili kuwabaini wahalifu na kufikishwa katika vyombo vyakisheria. Aidha Baraza linavitahadharisha vyombo hivyo kuepuka kufanya kazi yaokwa kusukumwa na matashi binafsi, jazba, chuki, matashi ya baadhi ya wanasiasana viongozi wa Dini pamoja na shindikizo la baadhi ya vyombo vya habari.

4. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linalaani na kupinga kwa nguvu zake zote kauli aliyoitoa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania na baadhi ya vyombo vya habari kuihusisha Zanzibar na ugaidi kutokana na tukio la kuuliwa Padri Mushi. Kauli hii inaonesha kuwa Mheshimiwa Waziri anaibagua Zanzibar katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu tunavyoelewa sisi suala la usalama wa nchi ni suala la Muungano hivyo huwezi kuihusisha Zanzibar pekee na suala la ugaidi. Hivyo, Baraza linaona kuwa kauli hizi zinazotolewa ni mbinu za makusudi za kuichafua Zanzibar katika Jumuiya ya Kimataifa kutokana na chuki binafsi dhidi ya Zanzibar na watu wake.

5. Aidha Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linamtaka Mheshimiwa Waziri kwa kulinda heshima yake kuwajibika kwa Watanzania kwa kujiuzulu kutokana na kushindwa kulinda usalama wa wananchi wakiwemo viongozi wa Dini ambao ndio walezi wa jamii.

6. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linalaani kauli za uchochezi zinazoendelea kutolewa na baadhi ya vyombo vya habari zinazochochea chuki, uadui, uhasama na mtafaruku kati ya Waislamu na Wakristo na kusahau kuwa Waislamu wameishi na Wakristo kwaamani, mapenzi na mashirikiano hapa Zanzibar karne na karne. Baraza linaona kuwa vyombo hivyo vya habari vinatekeleza ajenda ya kuivuruga Zanzibar kwa kuchochea vita vya kidini ili kufikia malengo yao wanayoyajua wenyewe. Hivyo, Baraza linaiomba Serikali kuvidhibiti kwa kuvichukulia hatua vyombo vyote vinavyotumia matukio haya kuchochea uadui na chuki kati ya Waislamu na Wakristo.

7. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linaviomba vyombo vya habari vya Zanzibar kuwajibika kwa Wazanzibari wanaolipa kodi kwa kuwapasha taarifa sahihi juu ya matukio muhimu yanayotokea katika jamii yao badala ya wananchi kutegemea kupokea taarifa za upotoshaji na uchochezi kutoka katika vyombo vya habari visivyotutakia mema.

8. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linaziomba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar kuwasilisha kwa Watanzania taarifa ya wazi ya matokeo ya uchunguzi wa matukio haya kwa kuanzia na lile la kumwagiwa tindi kali Sheikh Soraga, kupigwa risasi Padri Ambrose Mkenda, kuuliwa Padri huko Musoma, kupigwa risasi na kuuwawa Padri Mushi na kushambuliwa kwa mapanga na kuuliwa Sheikh Ali Khamis Bin Ali Khatibu wa Mwakaje.

9. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linawaomba Wazanzibari wote kuwa watulivu katika kipindi hichi ambapo upelelezi wa matukio haya ukiendelea. Aidha Baraza linawasihi Wazanzibari wote bila ya kujali tofauti zao za kidini kulinda umoja wao na kudumisha amani pamoja na kukataa kugawanywa ilikuwatoa katika ajenda yao ya msingi ya kudai Mamlaka Kamili ya Zanzibar katikaMuungano.

MOLA WETU MTUKUFU TUNAKUOMBA UINUSURU ZANZIBAR NA WATU WAKE DHIDI YA MAADUI WANDANI NA NJE WASIOITAKIA MEMA NCHI YETU

Imesainiwa na:

Sheikh Ali Abdalla Shamte

Amir wa Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar

19 wafariki katika ajali ya Puto Misri

Written By peterdafi.blogspot.com on Tuesday, February 26, 2013 | 2:10 PM



Zaidi ya watalii 19 wakiwemo waingereza na wafaransa ,wamefariki Kusini mwa Misri baada ya puto la joto walimokuwa kulipuka katika mji wa Luxor.
Ripoti zinaarifu kuwa kulikuwa na watalii ishirini katika puto hilo.
Moto na mlipuko vilisikika kabla ya puto hilo kuanguka Magharibi mwa Luxor.
Duru zinasema kuwa takriban maiti wanane walipatikana katika eneo la tukio.
Mji wa Luxor uko kwenye ukingo wa mto Nile, makao ya kale ya pharao. Ni eneo lenye sifa tele kwa watalii
Mwakilishi wa makamapuni manane ambayo yanatengeza putu hizo, katika eneo la Luxor alisema kuwa mlipuko wa gesi ulitokea wakati puto hilo likiwa umbali wa futi alfu moja kutoka ardhini.
''Kulikuwa na abiria 20 kwenye puto wakati wa ajali hiyo. Mlipuko ulisikika na abiria 19 wakafariki. Abiria mmoja na rubani wa puto hilo walinusurika,'' alisema mwakilishi huyo, Ahmed Aboud.
Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza iliambia BBC kuwa inatafuta taarifa kutoka kwa wenzao nchini Misri kuthibitisha taarifa za majeruhi waingereza.

Chanzo BBC Swahili

More Photos about JEDTT & Miss Tourism Taifa 2012/2013

Tone wa Tone fm na Miss Tourism at DSJ

 Gari iliyowabeba washiriki wa miss Tourism Taifa 2012/2013
 Mamiss wakishuka nakuwasilim katika viwanja vya DSJ eneo maalum kwa kuzindua safari ya JEDTT
 Mwenye nyeusi kati ni Gerard Ochali Rais wa wanafunzi DSJ (DASJOSO) Akinena jambo kwa wageni siku hiyo
 Tone alipata filsa yakusema jambo kwa Wanafunzi wa vyuo na wageni rasmi
Mwenye nyeusi shati ni waziri wa mahusiano Twaha akisema na wageni


 Wanafunzi wakiwa Level siti na full kipupwe tayali kwa safari ya Bagamoyo
 Zoura N aTone wanateta jambo mi sina tatizo nao wadau hawaaa

Mwanadada Mrembo sana ndani ya Gari kubwa lililokuwa limebeba Journalist tuu.

 Safari ilianza na hapa ni maeneo ya Tabata Matumbi
Waremboooooooooooooooooooooooooo na Pozzzzzzzzzzzz za Pic kwa Mr Blogger
Tabasam la Mshiriki wa Miss Tourism kwa dirishani safari ikiwa inaendelea.

 Foleni la Ubungo hapo. na ukitizama hizo Coasta zote hapo nyuma ni msafara wa JEDTT ni zaidi ya Gari nane

 Journalist wamejaa Gari la Kampuni ya LakeLand Africa na linalofuata lilijaa Mamiss na coasta zilijaa wanafunzi hakika ni Historia kwa chuo cha DSJ kuorganiz Evenyt kubwa kama hii haijawah tokea tangu chuo kianze.

Round About Mwenge
Baada yakufika Bagamoyo tulikatisha njia ya Mbegani ilin kutokea Kaole kijijini kwani piaq kulitokea tatizo la Gari za Lakeland Africa ni ndefu sana juu so mitaa ya Bagamoyo kwa njia ya magambani kuna nyaya za umeme ziko chini sana soo tulilazimika kuzunguka mara zote kwa njia ya Mbegani, washukuliwe Kampuni ya Lakeland Africa kwakweli.
Oooopppsss Mrembo anaejulikana kama Neema katia Pozzzz ndani ya Costar Mayai ni Bata tuuuuuuuu
Gari hili ndo kulikuwa na Vichaaa, masela, masimela, mahasla nk.....  naweza sema waenjoy kupita wenzao wote manake walijiachia sana sana mpakaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.............

Mapoz tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 Boda 2 Boda



Pale nyuma ni Mlezi wa wanafunzi Mr Bruda nani mwalimu wa DSJ, Mdada ni naibu waziri wa Michezo DSJ na kulia kwake ni Naibu waziri wa Katiba na Sheria DASJOSO

Pozzzzzzzzzzzz za Warembo
Baba lao Pierre Dafiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii na Majembe yangu hapo.
Polo, Tone, Mdada mwandishi, Jamaa na Pierre dafi
Mrembo CTY SIRAJI
 Muhifadhi wa makumbusho yataifa akitoa maelezo kwa wanafunzi
Baada yakufika Kaole
 Vijana na waandishi wakiandika Data

Warembo wakipita kwa kuhesabiwa
Wembo hawa watalipigania taji la miss tourism taifa mwezi wa tatu mwishoni.
Ni Neema kwa Pozzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz
Utulivu ni muhimu kwa kuskiliza na kuelewa vema
Wanatetaaaaa umbea sijuiiiiiiiiii sijui madini wanapeana hata sielewiiiiiiiiiiiiii 
Polo akiendelea na jukumu lakupiga Documentary ambayo itapatikana soon

 Warembo walipata fulsa yakupga picha katka Kaburi la Wapendanao
Majembeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
Neema, Mr Bruda na wanafunzi wengine
Pierre Dafi nikapiga picha katika kaburi la Wapendanao pia.
 Pozzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz kijanja weweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
Miti ya matumbawe
 Fucus deeep mzazi ukialibuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
Pierre Dafi na Polo
 Pierre Dafi na Polo ndo tulisimamia mzigo kama unavyooona
Vijana walienjoy sana bana
 Captainnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnnn
HD hand Cam on my Hand halitohalibika Jambo hata theluthhhh yake.
Pierre Dafi na Gerald Ochali 
 Sindo tukatia Swagg za Kisharooooooooooooooooo saasaaaaaaaaaaa
Nyomi la mandinga lilijaza uwanja wa DZ Restaulant chezea JEDTT weweeee
 Katika safari yoyote ile vituo vya gafla ni lazima hapa tulisimama kwa kujadili jambo

Mwenye rasta ni Neema na Rafiki yake
Napita tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
Neemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Pierreeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
Waremboooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
Neemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Miss Tourism na Mr Tone
Poz kwa Pozzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz
SANGODA NA MWENZIE
Miss Tourism na Mr Peter Dafi


 Maeneo ya Beach ya Millenium Hotel
Picha ya Viongozi
 Picha ya  Viopngozi na Mamiss
Ikawa na wanafunzi wengi wa Vyuo
Safari yakurudi kuondoka bagamoyo na kurudi Dar
Mrembo  Neema
Vijaaaanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 Wanarudi wakiwa wamechoookaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa chezea bata ndefu weewee

Pierre Dafi na Gerald Ochali
My Brother Tone
Warembo na poz za Dirishani
 Nikawekwa kati na kupiga picha
Mr Peter Dafi, Mr Chipungahelo na Polo

 Mr Peter Dafi, Mr Chipungahelo na Polo
Mr Tone wa Tone Fm na Brand zote za Yetu blogg huyu ndo mkali wao wengine wote wanafuata tuu. na mimi haonni mambo Dole tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger