Home » » CHADEMA NA SHINDANO LA KUTAFUTA NEMBO YA BAVICHA

CHADEMA NA SHINDANO LA KUTAFUTA NEMBO YA BAVICHA

Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, March 13, 2013 | 2:10 AM

 
Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) liko kwenye mchato wa kutafuta nembo yake ambayo itakuwa kielelezo cha vijana ndani ya CHADEMA. Nembo hii itakuwa alama ya utambulisho na inatarajiwa kutumika katika shughuli na mambo mbali mbali ya vijana ndani ya CHADEMA.

Katika kufanikisha upatikanaji wa nembo, BAVICHA inatambua uwepo wa vipaji mbalimbali vikiwemo vya ubunifu miongoni mwa vijana wa Tanzania ambao baadhi yao ni wanachama na wafuasi wapenda mabadiliko wa Chadema.

Ili kutoa fursa kwa vijana hawa kutumia vipaji vyao na kutoa mchango wao kwa Chama na Baraza lao, BAVICHA imeandaa shindano maalumu la ubunifu wa NEMBO YA BAVICHA na hivyo kukaribisha wale wote ambao wangependa kushiriki kwa kubuni nembo hii.

VIGEZO MUHIMU VYA KUZINGATIWA
Kwa wale wote wenye kipaji cha ubunifu na wangependa kushiriki shindano hili watapaswa kuzingaztia vigezo vifuatavyo katika ubunifu wao;
1. Rangi zitakazotumika ni lazima ziwe zinatokana na rangi kuu za CHADEMA
2. Nembo kuu ya Chama inaweza pia kutumika kubuni nembo ya BAVICHA
3. Mbunifu atoe maana halisi ya nembo atakayoibuni kwa mukhtadha wa vijana na maudhui mapana ya CHADEMA

MUDA WA SHINDANO
Muda wa shindano hili la kupata nembo ya BAVICHA utakuwa ni mwezi mmoja yaani kuanzia tarehe 26/02/2013 - 26/03/2013. Mbunifu anaweza kuwasilisha ubunifu wake moja kwa moja ofisi za BAVICHA zilizopo mtaa wa Togo Kinondoni – Manyanya, au kwa kutumia barua pepe: bavicha.chadema@gmail.com

MCHAKATO WA UCHAMBUZI
Baada ya wadau mbalimbali kuwasilisha nembo walizozibuni, Sekrataiati ya BAVICHA itazichmbua na hatimaye kupata nembo tatu bora ambazo zitawekewa utaratibu wa kushindanishwa na baadae kuingizwa kwenye vyombo vya kimaamuzi ili kupata nembo moja itakayotumiwa na Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA)

ZAWADI
Kwa kuwa shindano hili linalenga kuwapatia vijana wa CHADEMA na wasio wa CHADEMA lakini wenye mapenzi na CHADEMA fursa ya kutumia na kuvitangaza vipaji vyao na hivyo kutoa mchango wao katika ujenzi wa BAVICHA imara, mshindi wa shindano hili atapewa Shilingi 500,000/= kama zawadi na pia cheti maalumu cha kutambua mchango wake kwa BAVICHA.

WALENGWA
Walengwa wa shindano hili ni vijana wote wa CHADEMA pamoja na wanachama na wafuasi wa CHADEMA wenye ujuzi/kipaji cha ubunifu.

WITO
BAVICHA inawahamasisha vijana wa CHADEMA na wote wanaopenda mabadiliko kushiriki shindano hili ikiwa ni sehemu ya kuijenga taasisi hii ya vijana ndani ya CHADEMA

Imetolewa na:
Deogratias Munishi
Katibu Mkuu - BAVICHA
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger