HUKUMU
ya kesi iliyokuwa inamkabili staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja
na mumewe imetolewa leo na Hakimu Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, jijini Dar. Katika hukumu hiyo Kajala amehukumiwa kwenda
jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe
kwenda jela miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200.
Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini
na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe,
Faraji Agustino kukumbwa na msala wa kutakatisha fedha haramu.
Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na msala wa kutakatisha fedha haramu.
Post a Comment