Test Footer
HOME GROUND HOTEL SASA KUWA NA LIVE BAND KILA JUMAMOSI.
Written By peterdafi.blogspot.com on Monday, December 19, 2016 | 12:35 PM
HOME GROUND HOTEL SASA KUWA NA LIVE BAND KILA JUMAMOSI.
Hotel ya Kisasa nayakijanja ipatikanayo Sinza Mugabe, Kila Pamekuwa na Music Mzuri, Chakula na Vinywaji Bila Kusahau Vyumba Visafi na Vizuri kwa Kupumzika utokapo safarini ama kupumzika kama unahitaji utulivu.
HOM GROUND HOTEL Kwa sasa Kila Jumamosi Patakuwa na LIVE BAND .
Bila Kusahau Mechi Zote za Kimataifa Zitaonyeshwa ktk Luninga za Vyumbani na Zote zilizoko Bar na Restaurant.
Karibu sana Hom Ground Hotel Kila Siku kwa Chakula, Nyaa Choma, Vinywaji nk....!
Tamasha la ngoma za Jadi Kufanyika Tukuyu Mbeya na Naibu Spika Tulia
Written By peterdafi.blogspot.com on Monday, September 19, 2016 | 5:33 AM
TULIA:
Tukutane Tukuyu Mbeya Tarehe 07/10/2016.
TAMASHA LA NGOMA ZA JADI.
"Tuuenzi Utamaduni Wetu"
Sote tujumuike kwa pamoja.
27 January, Show Kabambe ya Ainea na Wasanii kibao Dodoma
Written By peterdafi.blogspot.com on Monday, January 18, 2016 | 11:13 PM
Gavanna wa Calfonia na Muigizaji Arnold amesema Muda umebadilika
Written By peterdafi.blogspot.com on Sunday, January 17, 2016 | 5:41 AM
MUDA UMEBADILIKA
Leo Arnold Schwarzenegger amepost picha hii na kusema Time Has Changed. akimaanisha kwamba Muda Umebadilika. Hakuweka picha hii ili mradi tu, aliondoka nyumbani kwake akiwa na mablanketi yake, akayapakiza kwenye gari na kwenda kupiga picha katika moja ya sanamu zake ikiwa imechongwa jinsi alivyokuuwa akitunisha misuli zamani.
Utajiuliza ni kwa nini! Anajua kwamba muda umebadilika, zamani, alikuwa kijana, muda mwingi alitumia akiwa gym, ila leo hii, muda umebadilika na inawezekana kuna baadhi ya vyuma hawezi kuvibeba.
Ana miaka 68 mpaka sasa hivi! Kila kitu kimebadilika, si yule wa kipindi kile, huyu ni mwingine kabisa, inawezekana sasa hivi hata kutembea kilometa 20 hawezi. Anatukumbusha kwamba muda unabadilika, unapopata nafasi ya kufanya jambo katika kipindi cha ujana wako, fanya kwani baadaye utakuwa umechoka, hautoweza kufanya biashara zako na kuzunguka huku na kule.
Ndugu yangu! Hakuuna muda ulio sahihi, muda wako ni sasa hivi, siku inayoitwa leo ndiyo ya kufanya mambo yako yote huku ukimtanguliza Mungu! Kumbuka kwamba, hata Arnorld alikuwa na nguvu, tena zaidi yako ila leo hii, hana nguvu, ila nyuma ya pazia, alitengeneza maisha yake, tena amefanikiwa zaidi.
JE UPO TAYARI KUTENGENEZA MAISHA YAKO SASA HIVI?
Serikali yafuta Gazeti la Mawio
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
IDARA YA HABARI - MAELEZO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
P.O. Box 8031, Dar es Salaam, Tel: 2110585, 2122771/3, Fax: 2113814, e-mail: maelezopress@habari.go.tz
Date: 17/01/2016
SERIKALI YALIFUTA GAZETI LA MAWIO
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kulifuta kutoka katika Daftari la usajili wa magazeti, gazeti lijulikanalo kama “MAWIO”. Amri ya kulifuta Gazeti hilo imetolewa kwa Tangazo la Serikali Na. 55 lililotolewa tarehe 15 Januari, 2016. Uamuzi huo umetolewa kwa mjibu wa Sheria ya Magazeti Sura ya 229, kifungu 25(1).
Hatua hii pia inazuia gazeti la Mawio kuchapishwa katika njia nyingine yoyote ikiwa ni pamoja na mitandao (Online publication) kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta Sura ya 306.
Serikali kwa masikitiko makubwa, imechukua uamuzi huu kutokana na mwenendo wa uandishi wa gazeti hilo usioridhisha wa kuandika na kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na kuhatarisha amani, utulivu na usalama wa nchi yetu.
Aidha, hatua hii ya kulifuta gazeti hilo imechukuliwa baada ya Msajili wa Magazeti kufanya juhudi kubwa za muda mrefu kuanzia Juni, 2013 hadi Januari, 2016 kumtaka Mhariri wa gazeti hilo kubadili aina ya uandishi wa habari na makala katika gazeti lake, bila mafanikio.
Msajili wa magazeti kwa juhudi zake alifanya mawasiliano na mhariri wa gazeti hilo mara nane kwa lengo la kutaka afanye marekebisho ya mtindo wa kutoa habari zake lakini mhariri wa gazeti hilo hakuzingatia ushauri mzuri aliopewa na Msajili wa Magazeti.
Ninatoa wito kwa wamiliki, wahariri, waandishi na watangazaji wa habari kuzingatia sheria, Kanuni na taratibu za taaluma ya uandishi wa habari ambazo zikizingatiwa hakutakuwa na migogoro yoyote. Aidha Serikali inasisitiza kwamba inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari unaozingatia maadili, weledi na Sheria za nchi na kwamba Serikali itaendelea kushirikiana navyo
Kwa upande mwingine ninatoa pongezi kwa vyombo vyote vya habari nchini vinavyozingatia maadili, weledi na Sheria zinazosimamia taaluma ya habari na sheria nyingine za nchi. Kwa namna ya pekee Serikali inawapongeza wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari ambavyo vinapofanya makosa vikielekezwa hujirekebisha na kutoa ushirikiano kwa Serikali na pia kubadili mwenendo wao; hawa ni pamoja na wahariri wa magazeti ya;
Mwananchi Tanzania
Mtanzania
The East African
Magazeti ya Daily News na Habari Leo
Uhuru na mengineyo
Ninapenda kusisitiza kwamba Serikali inapenda kujenga uhusiano mzuri na wa kirafiki kati yake na wadau wa sekta ya habari. Aidha ninasisitiza tena wadau wa sekta hii kuzingatia Sheria ili kujenga heshima ya tasnia ya habari na kulinda amani ya nchi yetu.
MWISHO
Imetolewa na Nape M. Nnauye(Mb,)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Dar es Salaam, leo tarehe 17 Januari, 2016
Picha jinsi kilivyohappen kwenye show ya selfie 16 na Koffi Olomide
Written By peterdafi.blogspot.com on Wednesday, December 9, 2015 | 12:44 AM
Vuna mbegu za kiume ukiwa na miaka18
Written By peterdafi.blogspot.com on Friday, June 26, 2015 | 8:02 AM
Daktari Kevin Smith, ambaye ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Abertay kilichoko Dundee Uingereza anasema kuwa baada ya utafiti wa kipindi kirefu amebaini kuwa ni bora kuvuna manii mapema ilikuepuka maradhi mengi yanayochangiwa na kuongezeka kwa umri.
Dakta Kevin Smith, anasema kuwa wizara ya afya ya Uingereza inapaswa kuunda hifadhi maalum ya mbegu za uzazi
Daktari Kevin Smith ameorodhesha ugonjwa wa akili ''autism'', na ule wa kuchanganyikiwa ama ''schizophrenia'' miongoni mwa magonjwa mengine mengi.
Dakta Smith, anasema kuwa wizara ya afya ya Uingereza inapaswa kuunda hifadhi maalum ya mbegu za uzazi ilikupunguza visa vya maradhi aliyoorodhesha.
Maoni yake hata hivyo yanapingwa na muungano wa wauguzi wa uzazi ambao wanasema kuwa hilo halitakuwa suluhisho la kudumu.
Badala yake shirika hilo linaitaka serikali ya Uingereza iweke sera zitakazowasaidia waingereza waliofikia umri wa uzazi kupata ajira.
Manii yakivunwa mapema yatasaidia kuepuka maradhi mengi tu
Takwimu zinaonesha kuwa wanaume wanaanza kupata watoto wakiwa na umri wa miaka 33 ikiwa ni ongezeko kutoka kwa miaka 31 katika miaka ya tisini.
Akitetea wazo lake katika jarida la madaktari la ''The Journal of Medical Ethics, Dakta Smith nasema kuwa wale wanaotaka kupata watoto mapema basi wafanye hivyo lakini kwa wale ambao wamegonga maiaka 40 ni vyema watumie mbegu walizohifadhi kwa matokeo mazuri zaidi.
Profesa Adam Balen, wa shirika la British Fertility Society, ameonya kuwa mbegu ziliyohifadhiwa huwa hazina nguvu kama zile zinazotolewa moja kwa moja.
Amebaini kuwa ni bora kuvuna manii mapema ilikuepuka maradhi mengi yanayochangiwa na kuongezeka kwa umri.
''Kwa mtazamao hawa vijana wanahitahitaji ajira na wapenzi basi watapata watoto pasi na matatizp yeyote.''alisema Profesa Balen
Wakati huo huo mwanasayansi mwenza Sheena Lewis, aliwashauri wanaume waanze kushughulikia swala la familia mapema katika ujana wao.
''ninataka kuwaelezea wazi kuwa umri mzuri wa kuzaa kwa wanaume na wanawake ni kati ya miaka ya 20 na 30."
Miss Tanzania Sitti Mtemvu Aivuruga Morogoro
Written By peterdafi.blogspot.com on Saturday, January 10, 2015 | 9:38 AM
Miss Tanzania aliyejivua taji City Mtemvu yupo ziarani mkoani morogoro..
dhumuni ya ziara ya City Mtemvu mkoani Morogoro ni kwenda kusalimia na kutembelea ndugu zake pamoja na kuhamasisha shughuli za kijamii.
City ambae kwao ni morogoro. amepokelewa na umati wa wanamorogoro ambao ulifurika maeneo ya mgahawa maarufu wa coco beach ambapo alihutubia mamia ya wananchi wa moro waliofurika kumpokea.. mnamo saa moja na dakika ishirini jioni
City alisisitiza sana kudumisha amani na mshikamano wa taifa.
Mkurugenzi mtendaji wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Tanzania environment conservation and welfare association (TECOWA) Sir c,de Heri Hoza amesema kuwa asasi yao imemteua City kuwa balozi wa kampeni ya utunzaji wa hifadhi asilia ya milima ya uluguru tao la mashariki.
Hoza amesema, kwakuwa asasi hiyo ina makao makuu mkoani Morogoro, wameona ni vema kumpa heshima hiyo bint wa nyumbani..
City usiku wa leo atajumuika na wanamoro ktk part ya pamoja kwenye club maarufu mjini hapo iitwayo viber na baada ya kumaliza xiara yake kisha atarejea jijini dsm kuendelea na shughuli zake.
Kauli ya Flora Mbasha Kufuatilia Kudai Taraka yake Rasmi.
Written By peterdafi.blogspot.com on Monday, January 5, 2015 | 4:27 AM
KAULI YA FLORÀ MBÀSHA KUFUATIA KUDAI TÀLAKA RASMI:
Nimefikia uamwuzi wa kudai talaka kutokana na kuchoshwa na vitendo vya ukatili nilivyokuwa nafanyiwa na mume wangu, kwa zaidi ya miaka8 na hata sasa bado anaendeleaje, Kwani hata kuongea uongo kwenye media juu yangu ni ukatili pia.. nimekuwa nikinyanyaswa kijinsia na mume wangu na sikuwahi kutoa taarifa mahala popote kutokana na vitisho alivyokuwa akinitisha. Watu Wengi wanafikiri nilikuwa na ndoa nzuri sana lakini kumbe nilikuwa Nikivumilia tu Kwani niliamini IPO siku atabadilika maana nilimpenda sana mume wangu.. Nilijaribu kuficha huzuni na maumivu yangu kila nilipotoka na mume wangu kwenda kwenye Huduma au mahala pengine penye mkusanyiko wa watu. Sijawahi hata Mara moja kutoa taarifa hata kwa wazazi wangu juu ukatili niliokuwa nafanyiwa na mume wangu.. Kwanza sikutaka kumvunjia heshima kwa ndugu zangu na pia alikuwa akinitishia kuniua na kuongeza kunifanyia ukatili huo.. Kutokana na historia yake ya nyuma alikuwa na uwezo wa kunifanya chochote na ndiyo maana nilikuwa nikimwogopa sana.. Siku zote nilikuwa akilala na panga kitandani ambalo ndilo alikuwa akinipiga nalo na kuapa kunichana chana Mwili Kabla ya kuniua.. Kipigo hicho nimekuwa nikikipata hata ninapokuwa kwenye Huduma bila kujali natakiwa kuwa kwenye mood nzuri ili ni perfome vizuri. Nimevumilia muda mrefu lakini ndo mateso yakawa yanazidi na kufikia hatua ya kufukuzwa akidai yeye ana mwanamke mwingine wa dini yake ya zamani Hivyo anataka amlete hapo nyumbani.. Nilikataa kuondoka na kumwambia amlete tu, tutaishi wote mimi nitakuwa nikilala chini maana nshazoea siku zote Amekuwa akinilaza chini . alivyoona siku zinazidi kwenda na mimi nimegoma kuondoka basi akaamwua sasa isiwe siri ya chumbani tena Akawa ananitoa ananipigia sebuleni na anasema nataka mtoto na wengine wote wajue kuwa huwa nakupiga humu ndani.. Ikafika hatua anataka kunitoa nje ya geti ili majirani wajue kuwa huwa napigwa na anifukuze mbele yao..
Kwa Miaka yote alinizuia kufungua account bank na kudai kuwa yeye ndo Mwanaume Hivyo pesa zote ataweka yeye. So pesa zangu zote nilizokuwa naingiza alikuwa akichukuwa yeye na kuzihifadhi kwa account yake binafsi.. Sikuwa nikibaki hata na mia.. Nilijaribu kufanya biashara lakini napo pesa zote Akawa akichukuwa yeye ikabidi niache.. Nikitaka hata vocha ya mia tano Lazima nimwombe hela na niitolee Maelezo ninampigia nani. Mume wangu kwa kipindi chote hakuwahi kuwa na kazi yoyote zaidi ya kunifanya mimi ndo biashara yake. Lengo lake ilikuwa ni kunitumia mimi kwa maslahi yake na sio upendo kama mke wake. Hakuwahi kunipenda hata yeye mwenyewe hukiri kuwa alinioa tu basi ili afanikiwe kwenda ulaya kwa kuwa mimi nilikuwa nikisafiri na babu yangu.. Na yeye kila akijaribu kwenda nje anashindwa. Kuna mambo mengi ya ukatili aliyokuwa akiyafanya ndani siwezi kuyasema kwa ajili ya maadili na pia bado Ninamheshimu kama mzazi mwenzangu. Alipoona siondoki pamoja na vipigo, matusi na kunifukuza kote.. Akasema nitahakikisha nakufanyia jambo ambalo utaondoka mwenyewe humu ndani bila kupenda.... Sitaki kuzungumzia swala ambalo liko mahakani ingawa hilo nahic ndilo alilokuwa kadhamiria ili tu niondoke. Nilijaribu sana kumsihi tukae kikao na wazee ili watushauri na kutusaidia lakini nilikuwa nikiambulia matusi tu ya nguoni ambayo siwezi kuyaandika hapa.. Siku niliyoondoka nyumbani alidhamiria kuniua alidai hata akiniuà hakuna atakaye amini kuwa ni yeye kaniua, na ni kweli maana sikuwahi kushtaki mahala popote. Alichukuwa panga akanipiga nalo kisha akaniniga Hadi nikaishiwa nguvu . Aliponiachia sielewi nilitokaje ndani. Ugomvi mkubwa ulitokana na mimi kukata kufanya tenda la ndoa kinyume na maumbile. Amekuwa Alinipiga na kunilazimisha kufanya tenda hilo kinyume na maumbike kwa Miaka msingi lakini nikisema bora nife kuliko kutendewa ukatili huo.Amekuwa akidai kuwa wanawake tumeumbwa ili tufanyiwe tenda hilo la ndoa mbele na nyuma so ni haki yake..
Niliondoka kwake nikiwa na sh elfu mbili tu. Nilimwachia kila kitu nyumba gari na pesa zote zikiwa kwa account yake zaidi ya milioni 50.
Sikuwa na uwezo wa kutoa pesa maana ni account yake binafsi.. Nimejitahidi sana kumwita kwenye vikao hata vya familia ili tu tujaribu kuzungum za lakini Amekuwa akionyesha dharau tu na kusema yeye haitaji ndoa tena anaoa mke mwingine Hivyo Hawezi kusuluhishwa. Ingawa Amekuwa akidanganya sana kwenye media. Nilimwuliza Unapata faida gani unapodanganya watu kuhusu mimi.. Akasema yeye amechafuka kwa ubakaji so acha na mimi nichafuke na akasema atahakikisha sifanyi Huduma sehemu yoyote labda nihame nchi. Kama msg hizo angekuwa amezituma bila kuandika na matusi ningezikopi but zaidi kauli zake ni za matusi. Hivyo imefika mahali nimeona bora tuachane kisheria na pia nipate haki yangu maana mume wangu anajivunia Mali ambazo hakuzitolea jacho yeye na huku anawatapeli watu kwa kudai kuwa hana pesa maana mimi nimeondoka nazo wakati ni uongo mtupu. Mimi ninapanda daladala siku hizi sababu sina uwezo wa kuwa na gari Hadi niazime kwa marafiki zangu. Mume wangu amekataa hata kumsomesha mtoto sasa hivi nahangaika kutafuta ada ili mtoto arudi shule lakini pesa yote anayo anayo mbasha. sasa sijui hapo ananikomesha mimi au mwanaye.!maana urithi wa mtoto ni elimu bora na mzazi anayempenda mwanaye atapambana ili kuhakikisha mtoto anapata elimu bora.
Nilikaa kimya muda mrefu sikutaka kuzungumza lakini imefika mahali Nimechoka maana huyu bwana hajiheshimu. Tukikutana anasema sio yeye anayepeleka habari mitandaoni..
Ninaomba wanaume wenyewe Mfano wake waache kuwafanyia ukatili wake zao majumbani .. Najua wako Wengi sana wanao nyanyasika kama ilivyo kuwa kwangu lakini Hawana sehemu za kukimbilia Hivyo wanavumilia tu na mwisho wa siku wanakufa na kuacha watoto wakiteseka. Mimi Nilivumilia zaidi ya Miaka 8 lakini imefika mahali enough is enough. Maandiko matakatifu yanasema, ndoa haivunjwi isipokuwa kwa uasherati. Acha nife kwa mapenzi ya mungu na sio kwa mapenzi ya mtu.. Na ni naamini sitakufa mpaka ndoto zangu zitimie.. Mume wangu ameapa kuwa atahakikisha sifanyi Huduma tena.. Lakini ninasema katika Jina la YESU, kama Bwana aishivyo, mwanzilishi wa Huduma yangu ni Mungu Hivyo mmalizaji wa Huduma yangu ni Mungu mwenyewe. Na sasa ninajipanga kumwimbia Mungu kama sitaimba tena.. Wakati mwingine usipokuwa mwangalifu ndoa inaweza kukukosesha ufalme wa mbinguni hasa Uki ingia kwenye ndoa isiyo sahihi. Ninampenda sana mume wangu lakini ninampenda Mungu wangu zaidi. Ahsante..
Nimeamwua kuandika Maana Nimechoka kuficha maovu aliyokuwa akinitendea.. Nimemtunzia heshima muda wote maana sikutaka jamii imjue ni mtu wa aina gani but yeye anatumia ukimya wangu kama udhaifu so naona bora niweze wazi ili jamii imtambue
Mimi yamenikuta najua Wapo Wengi tu wanapitia mateso niliyoyapitia mimi.. Kutokana na vitisho wanaendelea kunyanyaswa. That is not fair kwa kweli.. Mimi ningekufa Kabla ya wakati wangu lakini namshukuru mungu Niko hao hata sasa.
Na pia ili kuwaonya wanaume wanaume wenyewe tabia kama yake.. Kama umemshoka mwanamke achaneni kwa amani sio kumnyanyasa mwanamke kama alivyokuwa anafanya mbasha kwangu. Ninapinga vikali unyanyasaji wa wanawake na watoto majumbani











































