Home » » KIJANA ACHOMWA KISU AKITOKA DISCO

KIJANA ACHOMWA KISU AKITOKA DISCO

Written By peterdafi.blogspot.com on Saturday, March 2, 2013 | 6:20 AM

kijana  Godfrey Masharo  mkazi  wa mjini Iringa  akivuja damu  baada ya  kuchomwa kisu kifuani na watu  wasiofahamika  usiku  wa leo  wakati akitoka  kujirusha disco





Hivi  ndivyo  alivyochomwa  kisu  kijana  huyo.

  Hapa  akivuja  damu akiwa nje ya  kituo cha  polisi kabla ya  kupelekwa hospitali ya mkoa  wa matibabu  zaidi

WATU  wasiofahamika   wamemvamia na  kumchoma  na kitu  chenye  ncha kali  kifuani mkazi  wa mjini Iringa Godfrey Masharo (pichani) .

Tukio hilo  limetokea jana usiku majira ya saa 11 alfajiri  wakati  kijana  huyo akitoka  kujirusha katika  kumbi  za starehe mjini  hapa.

Akizungumza kwa  tabu na mtandao huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com kijana  huyo anadai kuwa watu hao  watatu ambao hawafahamiki  kwa majina  walimvamia na kumchoma na kitu hicho chenye ncha kali kifuani na kukimbia .

Alisema  kuwa  tukio  hilo  limetokea eneo la Miyomboni barabara  kuu ya Iringa -Dodoma jirani na jengo la Hazina Ndogo ya  mkoa  wa Iringa .

Hata  hivyo  alisema  kuwa  msaada  wake  ulitoka kwa  wasamaria  wema ambao  walimkuta  eneo hilo akiwa ameanguka kwa  kupoteza fahamu na kukimbizwa  katika  kituo cha polisi kabla ya  kupelekwa Hospitali ya  rufaa ya mkoa  wa Iringa kwa matibabu  zaidi .
NA FRANCIS GODWIN BLOG
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. peterdafi - All Rights Reserved
Template Created by Eddie Sucre Published by Bongoclanblog
Proudly powered by Blogger